Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kutumia siku ya kesho kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona.
Kupitia salamu zake za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Muungano kwa Watanzania alizozitoa leo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli aliwatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku akiwakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19) ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima.
“Watanzania wote watumie siku ya kesho kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona,”amesema Dkt. Magufuli.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi