Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM
TAASISI ya Tuse kimara Mavurunza jijini Dar es Salaam imeendesha mdahalo maalumu wenye lengo kuwaelinisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Mdahalo huo ulifanyika katika ukumbi wa bogeti Mavurunza ambapo watu mbalimbali walishiriki kwa kutoa maoni na mapendekezo yao huku mada halisi iliyokuwa ikisema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wanatambua umuhimu wa kujiandikisha.
Akizungumza katika mdahalo huo Spika wa bunge la vijana Taifa na kada wa chama cha CCM Antipas Pamba amesema zoezi Hilo linaumuhimu mkubwa kwa serikali kuweza kujua takwimu za wakazi wa eneo husika watakaoshiriki katika zoezi la upigaji wa kura.
“Zoezi la kujiandikisha ni muhimu kwa serikali kuweza kutanbua takwimu sahihi za wakazi waishio kwenye maeneo hayo lakini kutambua mikakati,miundo mbinu na namna itakavyo kuwa siku ya upigaji wa kura,” amesema Antipas
Aidha kada huyo amesema mchakato huo unalengo la kuwapa ufahamu,kipi lini,mambo gani yanayohitajika katika uchaguzi huo mdogo na uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake meneja wa TAASISI hiyo Albert Soriyambingu amesema mchakato huo unalengo la kuihamasisha jamii kulielewa zoezi la kujiandikisha kuwa ni demokrasia kwa watu wa vyama vyote.
Amesema kila mtu anahaki ya kumchagua kiongozi yeyote ampendaye aliyejitokeza kishiriki kinyanganyiro cha uchaguzi katika nafasi Fulani ya uongozi.
Nae mkurugenzi wa Tuse Cosmas Mgonange amesema kuzijenga fikra za wananchi ni kitu cha msingi ambapo kikatiba ni jambo muhimu wameahidi kuendesha midahalo sehemu mbalimbali ya kata ya kimara.
Amesema Ili kuondoa manung’uniko miongoni mwetu kila moja wetu ahakikishe anashiriki uchaguzi kwa kugombea ama kumchagua anayemuona anafaa katika nafasi Fulani.
More Stories
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini