November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tupike kisasa kuepuka magonjwa- Waziri Gwajima

📌 Atahadharisha kemikali zilizopo kwenye baadhi ya miti

📌 Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vyaanza kupika kisasa kwa kutumia Nishati Safi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa rai kwa Watanzania kupika kisasa kwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuepukana na magonjwa yanayosababishwa na moshi wenye kemikali zitokanazo na nishati chafu kama mkaa na kuni.

“Mkaa unapatikana kutokana na miti kukatwa, sasa ipo miti mingine ina sumu na mkaa unaweza ukawa umepatikana kutoka kwenye miti hiyo, hivyo kuathiri afya ya mtumiaji.” Amesema Dkt. Gwajima

Amezitaja sumu zinazotokana na miti kuwa ni pamoja na carbon dioxide na carbon monoxide hivyo mtu anapovuta moshi unaotokana na kuni na mkaa, moshi huo huenda kwenye mapafu na kusababisha oxygen kwenye damu kupungua.

Kuhusu ladha ya chakula kupungua kutokana na kutumia nishati safi ya kupikia, Dkt. Gwajima amesema matumizi ya nishati safi katika kupikia hupelekea chakula kuwa kitamu na kisichokuwa na harufu ya moshi.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum ina vyuo nane vya Maendeleo ya Jamii ambapo viwiili tayari vinatumia nishati safi ya kupikia.