January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tunda awapa makavu wanaomzushia ana Mimba

Na Mwandishi Wetu, TimeMajira Online

VIDEO vixen maarufu hapa nchini Tunda Sebastian maarufu kama ‘Cappuccino_tunda’, amewapa makavu wale wote wanaomzushia kuwa ana mimba na amewataka wafuatilie mambo yao kuliko ya watu wengine ambayo hawana uhakika nayo.

Akiwapa makavu hayo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Tunda amesema, amechoshwa sana na kuzushiwa kuwa ana mimba kwani sio Ugonjwa ambao unaweza kumfanya mtu afiche ikiwa yeye ni mwanamke.

“Kuna vitu vinachosha aisee!. Khaa kwani mimba ni ugonjwa hadi mtu ufiche?, sina mimba ndugu zangu siku nikiwa na mimba wala siwezi ficha, maana ni jambo natamani!. Ifike mahali tuache kuzushiana mambo kupitiliza!,2 amesema Tunda.