Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
TUME ya Haki za Binadamu imesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao ,inajikita katika kuhamasisha jamii juu ya uelewa wa haki ya mpiga kura ya kuchagua na kuchaguliwa.
Afisa Uchunguzi kutoka Tume ya Haki za Binadamu Pontian Kitorobombo ameyasema hayo jijini katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere.
Amesema,lazima jamii inapojiandaa kuingia katika Uchaguzi Mkuu iwe na uelewa wa kutosha juu ya Haki zao ikiwemo kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili wapate haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.
Vile vile alisema Tume hiyo inajikita kuhamasisha wananchi kushiriki Mikutano ya kampeni Ili waweze kusikiliza sera za wagombea na kuwapima kwa hoja zao hatua itakayowawezesha kufanya maamuzi katika sanduku la kura.
“Jukumu la Tume ya Haki za Binadamu ni kuangalia mchakato mzima wa Uchaguzi kama unafuata Sheria na taratibu kuanzia kujiandikisha ,kuteuliwa,kushiriki kampeni hadi zoezi la Uchaguzi maana Uchaguzi unafanyijankwa mujibu wa Sheria,kwa hiyo Kila hatua lazima ifuate Sheria,
“Kwa hiyo Tume inaangalia kama taratibu zilizoainishwa zinafuatwa na wananchi wamepata Haki zao.”amesema Kitorobombo na kuongeza kuwa
“Hivyo Tume inaangalia kama Kuna malalamiko Kutoka kwa wananchi ya kunyimwa Haki ya kujiandikisha,kunyimwa Haki yao ya kuchaguliwa/kugombea,inayapokea na kuyafanyia uchunguzi na kutoa ushauri kwa mamlaka husika.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Sheria Kutoka Tume ya Haki za Binadamu Andrew Samanyi amesema wameshiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa Elimu ya masuala ya kisheria,Haki za Binadamu na misingi ya utawala Bora kwa wananchi .
Aidha amesema ,majukumu ya Tume hiyo yapi kwa mujibu wa Katiba ambayo imeipa Tume Mamlaka ya kupokea malalamiko yanayohusu uvunjifu wa haki na ukiukwaji wa misingi ya utawala Bora.
hata hivyo amesema jukumu Kuu ni kuhamasisha na kihifadhi haki za Binadamu na Utawala Bora.
Simanyi ametaka majukumu mengine ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuwa ni pamoja na kufanya tafiti zinazohusu masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ili kutoa ushauri kwa Serikali kuona nini kinaweza kufanyika kwenye masuala hayo.
Pia amesema Tume hiyo ina jukumu la kupitia Sheria mbalimbali ambazo zinakuwa zinatungwa na kuona namna gani Sheria hizo zinapokuwa zinatungwa zinazongatia masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
“Pamoja na hayo pia tunafanya ziara magerezani ,Vituo vya polisi na maeneo mengine ambayo watu wamezuiliwa na kuangalia kwa namna gani Tume inaweza kuishauri Serikali katika kuboresha mazingira ya wafungwa .”amesema Samanyi
More Stories
‘Valentine day’kutumika kutangaza mapango ya Amboni
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa