Na Queen Lema, TimesmajiraOnline,Arusha
Chama cha Akiba na Mikopo cha Tumaini, (Tumaini Saccos) kimefanikiwa kutoa mikopo ya bilioni 11 kwa wanachama 1900 wa chama hicho huku lengo likiwa ni kuwasaidia kuweza kutatuta mambo mbalimbali ndani ya jamii zao.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Tumaini Saccos Flora Balige, wakati akizungumza na waaandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya chama hicho kwenye maonesho ya wiki ya fedha yanayoendelea jijini Arusha.
Amesema kuwa chama hicho kimeweza kufikia katika hatua hiyo kwa kuwa wameweza kuweka nidhamu mbalimbali za kifedha kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kutoa elimu zaidi.
Amefafanua kuwa chama hicho kimeweza kuwa na faida kubwa na kimeleta maendeleo katika Mkoa wa Arusha hususani nyaja za uchumi kwa kuwa kinaangalia zaidi mahitaji ya wanachama.
“kila mara huwa tunatoa elimu hii ya fedha aina za mikopo tulizonazo imesaidia sana wanachama wetu kuweza kufikia malengo yao kwa haraka lakini pia kuweza kukipenda chama chao hata kuwafuatilia maendeleo kwa karibu sana,”amesema.
Hata hivyo amewataka Watanzania ambao wanafanya kazi katika taasisi au mashirika mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatumia fursa hiyo kwa kuungana pamoja na kisha kuweza kunufaika na huduma za mikopo ambazo zinatolewa.
More Stories
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia