Na Esther Macha, Timesmajira Online, Kyela
WAATHIRIKA mafuriko katika kitongoji cha Lugoje kata ya Mwaya wilayani Kyela mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwapatia maeneo ya kujenga nyumba ili kuepukana na adha ya mafuriko ambayo ikijitokeza kila mwaka.
Kauli hiyo wameitoa jana April 23,2024 wakati wakati Taasisi ya Tulia Trust ilipowatembelea na kutoa msaada wa vyakula vilivyokabidhiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela.
Akizungumza na waandishi wa Mwathirika wa Kitongoji cha Lugoje kata ya Mwaya ,Estelia Simon amesema kuwa mafuriko yalitokea usiku wakiwa wamelala na kulazimika kukimbilia kanisani na barabara.
” Tumekaa kanisani wiki nzima kwa sasa tumerudi katika nyumba zetu na katika mafuriko hmaafa haya yalikuwa mazito mpunga wote tuliokuwa tumelima umeteketea na maji na kuoza”amesema .
Ameiomba serikali
kuwaangalia kwani kuna maeneo mengi yapo wazi kugaiwa wapewe ili waweze kujenga makazi ya kuishi ili kuepukana na changamoyo za mafuriko.
Kwa upande ofisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust ,Joshua Mwakanolo ambaye alimwakilisha Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Rais Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) Dkt.Tulia Ackson amesema baada ya kupata taarifa za maafa hayo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Kyela,Ally Mlaghaila na kuwatoa kutoa taarifa Mkurugenzi wao.
Ametaja msaada wa vyakula uliokabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Kyela,Josephine Manase kwa ajili ya waathirika kuwa ni Mchele kilo 300, Maharage kilo 50, Sukari kilo 75 pamoja unga wa ugali kilo 125.
Mratibu wa maafa halmashauri ya wilaya ya Kyela,Amos Kayendele amesema athari kubwa imejitokeza katika mashamba ya mpunga,migomba ambayo ndo tegemeo kwa wananchi wa kata za Mwaya ,Matema,Bunjonde,Ngonga,Katuma Songwe ,Kanjunjule ,Tala Tala.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine amesema wilaya ya Kyela ilikubwa na Mafuriko mwishoni mwa mwezi March mwaka huu .
“Tunamshukuru sana serikali kwa kutupatia msaada wa mil.35 lakini leo hii tumepokea msaada mwingine kutoka Taasisi ya Tulia Trust tunasema asante”amesema mkuu huyo wa wilaya.
Venusta Mpogole ni Ofisa Mtendaji kata ya Mwaya amesema kuwa katika maafa hayo hakuna vifo vilivyotokea na kwamba kata ya Mwaya ina vijiji 10 ambavyo vyote vimeingiliwa na maji kwa kiwango tofauti na kusema katika kata ya Mwaya vijiji 264 vimeingiliwa na maji na mpaka Sasa wamebakiwa na Kambi moja ambapo awali kulikuwa na Kambi 10 za waathirika wa mafuriko hayo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa