Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
SPIKA wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson amepokea msaada wa mifuko ya saruji 610 yenye thamani ya milioni 10.3 kwa ajili kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya upasuaji wa kibingwa katika hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Msaada huo umetolewa na mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mkoani Mbeya,Maseke Wambura ambaye ndugu yake aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo na baada ya kupona aliona changamoto ya ujenzi na kuchukua uamuzi wa kutoa msaada huo ili uweze kusaidia ujenzi huo wa vyumba vitatu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya , Dkt.Godlove Mbwanji amesema kuwa upasuaji wa moyo ,ubongo na mishipa ya fahamu ni huduma ambazo zilikuwa zikipatikana jijini Dar es Salaam hospitali ya Jakaya Kikwete kwa upande wa moyo.
‘’sisi sote tunafahamu kwamba nchi yetu ni kubwa sana kumtoa mgonjwa hapa kumpeleka jijini Dar es Salaam ni gharama na wengi huwa hawawezi kufika kwa mfano kwa mwezi tunakuwa na wagonjwa 20 ambao wangehitaji upasuaji wa moyo na wanapatiwa rufaa kwenda Dar lakini unaweza ukaelewa katika hali ya uchumi ni wachache sana ambao wanamudu hizo grama na kwenda kutibiwa,”amesema Dkt. Mbwanji.
Amesema kuwa serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu hivyo wananchi na wadau wanatakiwa kuguswa kusaidia huduma za kijamii kama ambavyo mdau huyu alivyojitokeza kutoa mifuko 610 .
Dkt. Dinos Mwaja ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya ujenzi amesema kuwa watakuwa na jengo maalum la kuzibua mishipa ya damu na baada ya kukamililka jengo hilo wataweza kufanya upasuaji wa kifua , moyo,mishipa ya damu na ubongo na mradi huo unategemewa kutumia zaidi ya bilioni1 mpaka kukamilika kwake.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi