Na Penina Malundo,Timesmajira
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi huduma mpya iitwayo T. FIBRE kidijitali TRIPLE HUB,kifurushi kipya ambacho kimebuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya kizazi cha sasa ambacho kinajumuisha huduma tatu muhimu yaani mfumo wa “Kifurushi kimoja, Bili moja.
Huduma zitakazotolewa katika kifurushi hicho ni Intaneti (Unlimited Internet) kwa matumizi ya familia, ofisi, biashara, na hata mifumo ya kidigitali, Huduma ya Simu ya Mezani (Landline Voice Service) inayompa mteja fursa ya kupiga na kupokea simu kwa urahisi kupitia miundombinu ya Faiba na ya tatu ni Huduma ya Intaneti na Dakika kwa Simu ya Mkononi (Mobile Services) inayomwezesha mteja kupata vifurushi vyenye GB na Dakika za kutosha ambavyo vinaweza kutumika popote pale mteja alipo akiwa na Laini ya simu ya TTCL.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Promosheni kutoka TTCL,Janeth Maeda amesema Kifurushi hicho cha “Faiba Miangoni Kwako – T.FIBRE TRIPLE HUB” ni suluhisho kamili kwa nyumbani, Ofisi au biashara.

Amesema ni kifurushi kiichoundwa ili kurahisisha maisha, kupunguza gharama, na kutoa thamani kubwa zaidi kwa wateja wao.”Kupitia huduma hii, TTCL inafungua ukurasa mpya wa kidijitali chini, Shirika la kwanza Tanzania la mawasiliano kutoa kifurushi hiki kinachojumuisha huduma tatu kwa kwa pamoja “T.Fibre Triple Hub” lengo likiwa ni kuunganisha Watanzania wote kwa njia bora, rahisi na ya kisasa kwa gharama nafuu.
“Shirika linalenga kuhakikisha kila nyumba, kila ofsi, na kila Manyabiashara hapa nchini anakuwa sehemu ya mageuzi haya ya mawasiliano na hivyo kuunga mkono
agenda ya serikali ya kuongeza matumizi ya TEHAMA na kukuza uchumi kidigitali,”amesema

Amesema kifurushi hicho kipya kimeundwa kwa ajili ya wateja wa familia, taasisi, pamoja na mteja yeyote anayehitaji ubora na urahisi katika huduma za mawasiliano.
Maeda ametaja miongoni mwa faida zinazopatikana katika kifurushi hicho ni pamoja na Kifurushi hicho utumika kwa Wateja wote wawe wapya au walipo, wanaweza furahia huduma hii,Upatikanaji wa huduma zote tatu zinapatikana kwenye kifurushi kimoja,Gharama Nafuu pamoja na
Ubora na Uhakika popote ulipo kwa masaa 24 kwa siku zote saba mteja anapata huduma.
Ametaja gharama za kifurushi cha T-Fiber Triple Hub kinapatikana kwa gharama nafuu kuanzia shilingi 70,000 tu kwa mwezi ambapo mteja anapata manufaa makubwa kama Intaneti ya kasi kubwa bila kikomo (Unlimited Internet), yenye uwezo wa hadi
20 Mbps upload na 20 Mbps download – intaneti imara, ya uhakika, inayokidhi mahitaji ya nyumbani, kazini, na biashara.
Amesema uzinduzi wa T-Fiber Triple Hub siyo tu kutambulisha kifurushi kipya sokoni bali ni uthibitisho tosha kuwa TTCL inaendelea kusonga mbele – kubuni, kuboresha, na kuwekeza kwa nguvu katika mustakabali wa mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina