Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania limezindua rasmi huduma maalum yenye vifurushi vya intaneti vyenye Kasi ya ajabu ya “TTCL Faiba Supersonic Experience kwa lengo la kuwarahisishia huduma za Internet katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumbani na Ofisini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua huduma hiyo mbele ya waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL,Vedastus Mwita amesema watu wanahitaji kufanya biashara mtandaoni, kufurahia michezo ya mtandaoni,kufanya kazi zao kwa uhakika wakiwa nyumbani au Ofisi kwa kutumia mtandao uliokuwa imara kwa wakati wote.
Amesema huduma hizo zinahitaji Intaneti ya uhakika, yenye kasi kubwa ya TTCL Faiba Mlangoni kwako.”Ndiyo maana Shirika limeongeza thamani zaidi ya huduma zetu kwa kukuletea “TTCL Faiba Supersonic Experience; Kasi Balaa.” Hii ni huduma itakayomuwezesha mteja kufanya kazi zake bila ya kuwa na wasiwasi.

”Hivyo, TTCL inahakikisha kila mteja anapata uzoefu bora zaidi wa kidijitali,tunajivunia kusema kuwa kwa kiwango hiki cha kasi na ubora wa huduma, TTCL ndiyo chaguo la kipekee kwa wale wanaotaka kufurahia intaneti ya kweli ya kasi kubwa kwa matumizi ya Ofisi, Biashara au Nyumbani,”amesema
Aidha Mwita amesema ni wakati wa wateja wao sasa, kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali, kwa kuwa vifurushi vyao vinawahakikishia kupata huduma wanazostahili.” Shirika tayari lina miundombinu imara inayowezesha huduma hizi kutolewa kwa uhakika mkubwa kwa Watanzania wengi zaidi.
“Sasa ni mwendo wa Supersonic Experience” – kasi ya ajabu, kasi isiyopimika, kwa wateja wote wa huduma ya “Faiba Mlangoni kwako” hivyo ni wakati wa kufurahia intaneti ya kweli ya kasi kubwa mlangoni kwako,”amesema.

Mwita amesema TTCL imekuja na vifurushi vipya vya TTCL Faiba Supersonic Experience vinavyotoa nguvu ya kufanya kila kitu kidijitali bila mipaka.
Kuanzia Smart Home, Smart Office, gaming, streaming, biashara mtandaoni hadi mawasiliano ya uhakika.
Ametaja miongoni mwa vifurushi ambavyo TTCL vinavyo ni pamoja na T-Fiber BUSTA –,T-Fiber Triple Hub Plus ,T-Fiber Triple Hub Extra,T-Fiber Triple Hub.”
Wateja watakaojiunga na vifurushi vya T-Fiber Busta, T-Fiber Triple Hub Plus, T-Fiber Triple Hub Extra, T-Fiber Triple Hub Balaa na T-Fiber Triple Hub Jumbo watapatiwa ofa ya laini ya Simu ya Mkononi ya TTCL bure kulingana,”alisisitiza
Amesema vifurushi hivyo vipya vimeboreshwa ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya kisasa ya kidijitali ikiwemo kuongeza matumizi ya kidijitali nyumbani, ofisini au katika shughuli za biashara,Kucheza michezo ya mtandaoni,Kutengeneza na kusambaza maudhui ya kidijitali kwa ubora zaidi.
Mwita amesema katika kipindi cha mapinduzi ya kidijitali,TTCL inaendelea kuongeza ubora wa huduma zao ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wateja wao.

More Stories
Tanzania,Saudi Arabia zaimarisha ushirikiano sekta ya nishati
MISA wadau Summit kuibua fursa za maendeleo Iringa
FIFA na TFF yaanza utambuzi wa vipaji vya Watoto mkoani Rukwa