Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Yahya Ahmed Okeish yaliyolenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Machi 16, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ikiwemo mashirikiano ya kimkakati katika usalama wa upatikanaji wa mafuta, uendelezaji wa gesi, nishati safi ya kupikia, nishati jadidifu, pamoja na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu wa mafunzo kwa wataalamu, teknolojia ya uchimbaji wa mafuta na gesi pamoja na juhudi za kukuza sekta ya nishati kwa nchi zote mbili.




More Stories
Wizara,TPSF kuongeza ushiriki kongamano la kiswahili
Prof.Mbawara:TMA yakamilisha ufungaji wa mitambo miwili ya uangazi wa hali ya hewaÂ
PBPA yapongezwa kwa usimamizi wa upatikanaji wa Mafuta nchini