November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL yafanya maboresho katika huduma zake

Na Penina Malundo,Timesmajira

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limefanya maboresho makubwa katika mtandao wao wa simu kwa lengo la kurahisisha uharaka wa huduma bila vikwazo vyovyote kwa  watumiaji wa huduma zao.

 Akizungumza  na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,jana Mkurugenzi wa Biashara TTCL Vedastus Wambura, amesema maboresho hayo yamefanya mtandao kupatikana popote iwe mijini au vijijini na kufanya watumiaji wa mawasiliano kutumia teknolojia zao za kisasa.

Amesema maboresho hayo  ni chachu ya biashara hasa katika mitandao ya simu za mkononi na kumrahisishia mtumiaji kupata unafuu wa gharama pamoja na kupata vifurushi ambavyo vitatumika hadi mwisho badala ya kupewa muda maalum wa matumizi.

“ Tutahakikisha watanzania wanapata huduma zetu za TTCL vizuri ndio maana tumekuja na kampeni ya ‘Walete nyumbani mambo ni moto’,”amesema.

Amesema katika maboresho hayo wameweza kuleta vifurushi mbalimbali kwa wateja wao ikiwemo kifurushi cha Jiachie Extra,Buffer pamoja na kuboresha  kifurushi cha T Connect Plus.

“TTCL ndio kinara wa mawasiliano nchini hivyo uzinduzi wa kampeni hiyo maalum ya maboresho  ya teknolojia ambayo yatahakikisha mtandao unapatikana nchini nzima na data  za uhakika,”amesema. 

Amesema kampeni hii inalenga kufanya Dara kuwa ya uhakika na kurahisisha sauti  na kufanya mawasiliano kuwa ya bei nafuu bila kuwa na vikwazo vya kifedha.

 Kwa upande wake Claxton Chipando (Baba Levo)ambaye ataongoza kampeni hiyo amesema mawasiliano ya simu ndio msingi mkuu kwa jamii hivyo maboresho hayo yatasaidia kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa.

Amesema vifurushi hivyo vipya vitasaidia upatikanaji wa huduma kwa maeneo mbalimbal