Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
WANAWAKE wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) wameungana na Wanawake wengine kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa watoto wenye matatizo ya moyo waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( JKCI) kama ishara ya faraja kwao
Akizungumza kwa niaba ya wanawake zaidi ya 400 wa Shitika hilo leo Ofisa Uhusiano TTCL Adeline Berchimance amesema msaada huo ni utaratibu wa kawaida wa shirika katika kujali kazi na utu
” Kama tunavyofahanu kuwa kiongozi wetu wa nchi anahamasisha kufanya kazi kwa kujali utu wanawake wa TTCL tumeamua kumuunga mkono rais wetu Dkt Samia Suluhu katika usemi wake wa Kazi na Utu,” amesema Berchimance
Ameongeza kuwa TTCL katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2026 wameweza kuchangishana na kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto na wazazi waliolazwa JKCI
Aidha Berchimance amevitaja vifaa vilivyokabidhiwa JKCI kuwa ni pamoja na
Pampers,maziwa na taulo za kike ambazo zitawasaidia watoto, wazazi na walezi hospitalini hapo

Pia amewapongeza wauguzi na madaktari kwa kusimamia taaluma zao kwa kutoa msaada wa matibabu kwa kuzingatia utaratibu huku akiahidi kuwa wanawake wa TTCL wataendelea kujitoa kwa hali na mali katika kulinda na kuwafariji wagonjwa wa JKCI
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa Mbobezi magonjwa ya moyo kwa watoto na Daktari Bingwa Mbobezi magonjwa ya moyo kwa watoto Dkt. Naizihijwa Majani akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi amesema tatizo la moyo kwa watoto lipo na JKCI imekuwa ikitoa tiba sahihi
“Kati ya watoto 100 wanaozaliwa nchini mmoja au wawili wanagundulika kuwa na tatizo la moyo na kwamba ugonjwa huo upo katika makundi mawili,” amesema Dkt.Majani
Amesema katika watoto milioni 2 wanaozaliwa nchini kwa mwaka 16,000 wanakutwa na tatizo la moyo ambapo JKCI imekuwa ikiwahudumia kwa ufasaha ili kuokoa maisha yao

Dkt.Majani amezitaja dalili za magonjwa ya moyo kwa watoto kuwa ni pamoja na kutokukua vizuri, kuhema harakaharaka, kushindwa kunyonya, uzito kupungua, kukohoa mara Kwa mara, kuumwa kifua na utapiamlo
Amezitaja dalili zingine kuwa ni kifua kupanuka moyo kwenda mbio, kushindwa kucheza na wenzake, kushindwa au kuchelewa kutembea, kuchuchumaa mara kwa mara na kuchoka bila sababu
Amewaasa wazazi walezi na watanzania kwa ujumla wanapoona dalili hizi kwa watoto kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10