December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL na Burundi zasaini Mkataba kuongeza huduma kwenye Mkongo

Na Rose Itono, timesmajira

SERIKALI imeshuhudia utiaji saini mkataba wa kibiashara na kuongeza huduma kwenye mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL na Burundi

Akishuhudia utiaji saini huo Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema tukio hili linaashiria hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara na teknolojia kati ya nchi zetu mbili hizi

Amesema mbali na kuimarisha uhusiano wa kibiashara pia mkataba huu utafungua njia ya ushirikiano mpana zaidi katika sekta ya mawasiliano

“Leo hii tunashuhudia tukio la utiaji saini mkataba wa kibiashara wa kuongeza huduma kwenye mkongo wa mawasiliano kati ya (TTCL)na Burundi Backbone System (BBS) kupitia mkataba mpya wa kibiashara wa miaka mitano wenye thamani ya dolq za Kimarekani mikioni3.3 sawa na sh. Bilioni 8.3 za Kitanzania,” amesema Nnauye

Ameongeza kuwa uhusiano wetu na Burundi kupitia Burundi Backbone System ulianza mwaka 2019 wakati tulipoingia mkataba wa kwanza na kuwapa huduma.za mkongo kupitia eneo la Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi katika wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera na Manyovu upande wa Kigoma

“Tunaamini mkataba huu mpya utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania na Burundi kwa kuimarisha uchumi,biashara na ushirikiano wa kijamii,” amesema Nnauye

Aidha ametoa shukrani kwa Serikali ya Burundi na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora za mkongo wa Ta if a wa mawasiliano kwa lengo la kukuza maendeleo ya nchi

” Matokeo mazuri ya huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano yamesababisha Serikali
ya Burundi, kupitia BBS, kukubali kuongeza huduma hizo,” amesema Nnauye na kuongeza kuwa mkataba mpya utaimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Burundi na utaboresha mawasiliano kati ya nchi hizi mbili.

Amesema taifa tunajivunia mchango mkubwa katika kuboresha mawasiliano katika Afrika
Mashariki na kwamba mkataba mpya utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi
wa Tanzania na Burundi kwa kuimarisha uchumi, biashara, na ushirikiano wa kijamii.

“Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali ya Burundi na BBS kwa kuendelea kutuamini na
kutupa fursa ya kuwahudumia. Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora za Mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano kwa lengo la kukuza maendeleo ya nchi yetu na kanda ya Afrika Mashariki,” amesema .

Ameongeza ni kweli kabisa kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki inapaswa kuwa na mipango na
mikakati ya kuendeleza sekta ya mawasiliano ndani ya Jumuiya Kwa kujenga mifumo ya
kidijitali itakayowezesha Afya mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao, kilimo
Mtandao, serikali mtandao, na malipo kwa kutumia mifumo ya kidijitali ni muhimu sana
kwa kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wananchi .

Amesema serikali imeonesha dhamira thabiti ya
kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano ya kimkakati kama njia ya kufanikisha
maendeleo ya nchi.

“Malengo yetu hadi kufikia 2025, Mkongo wa Taifa uwe umefikia Km
15,000 umeunganisha Mikoa na Wilaya zote,” amesema na kuongeza kuwa upanuzi wa Mkongo wa Taifa ni mojawapo ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali
katika sekta hiyo na unatarajiwa kuleta faida nyingi kwa wananchi wa Tanzania ikiwa
pamoja na; kuimarisha uchumi, kuboresha, kuiunganisha na kuongeza ushindani wa kimaraifa.

Aidha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano una uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko
chanya katika nchi hizo na Kwa kuunganisha nchi hio kwa njia ya mtandao wa mawasiliano
wa kasi na wa kuaminika, innafungua fursa mpya za biashara, uwekezaji, na ushirikiano
katika nyanja mbalimbali.

Amesema SerikaliI kupitia TTCL itaendelea kuboresha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kuhakikisha unatoa
huduma bora kwa wananchi na wadau wote,

Pia ametoa wito kwa nchi nyingine za Afrika
kujiunga na mkongo huo ili kuweza kuunganisha bara zima la Afrika na kukuza uchumi kwa pamoja.

Kadhalika aliitaka TTCL kuhakikisha BBS wanapata huduma bora
na yenye uhakika kama ilivyoainishwa katika Mkataba uliosainiwa kati ya pande zote
mbili.

Amesema hiyo ni muhimu kwa sababu BBS inategemea sana huduma za TTCL ili kuendesha
shughuli zao kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mtendsji Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulangs amesema mkataba unaleta fursa nyingi za
kibiashara kwa mabenki, mitandao ya simu, na makampuni mengine yaliyopo Tanzania na kuyaomba mabenki, mitandao ya simu, na makampuni mengine
kuchangamkia fursa hiyo ya Mkongo.

Kadhalika alitoa ombinkwa Burundi kuona namna wanaweza kutumia kituo cha kuhifadhi data kimtandao (NIDC) Kwa kuhifadhi data zao kwenye kituo hiki salama na cha kisasa.

Naye Mtendaji Mkuu wa BBS, Jeremie Hageringwe amesema ni mkataba wenye kuleta manufaa baina ya nchi zote mbili na pia utatoa huduma rafiki na bora Kwa wananchi wa Burundi.

Amepongeza majadiliano yaliyowezesha kukamilika Kwa mkataba huo na kwamba serikali ya Burundi inahitaji BBS kutoa huduma Bora zenye ubora Ili kukuza uchumi.