January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL kuingia katika ushindani kibishara Soko la kidunia

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline, Dodoma.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL)
limesema kwasasa linaweza kuingia katika ushindani wa kibiashara katika Soko la Kidunia kutokana na sasa wameweza kuwafikia watanzania waliowengi waliopo vijijini ikiwa ni pamoja na kuwapatia bando za bei nafuu.

Akizungumza mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa,Dkt.Khamis Mkanachi alipotembelea katika banda la TTCL,jijini hapa leo katika maonesho ya 28 ya kilimo nanenane,Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya nzuguni Afisa biashara kitengo cha wafanya biashara wakubwa Frank Tibalerwa alieleza kuwa kutokana na ushindani wa kibiashara Shirika hilo kwa sasa linaweza kuwafikia wananchi waliowengi kwa kutumia mtandao kwa haraka na kwa bei nafuu.

“Mheshiwa Mkuu wa Wilaya TTCL kwa sasa  imejipanga kwa ajili ya kufanya mabadikilo makubwa hususani katika nyanja ya kibiashara na viwanda ndio maana tunapatikana hadi vijijini na mtandao huu huko vizuri hausumbui wa kukwama kwama na bando zetu ni gharama nafuu,”amesema Tibalerwa.

Amesema kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma hiyo hususani katika watu waishio vijijini wakiwemo wakulima kwa kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote.

Kwa upande wa Meneja Biashara TTCL Tawi la Dodoma Leila Kongwe ameeleza kuwa shirika hilo limejikita kuhakikisha limawapatia wanachi huduma muhimu kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika.

Kongwe amesema kuwa ili kuhakikisha TTCL imawafikia wananchi itahakikisha inawapatia vocha za uhakika pamoja na kuwapatia vifurushi vya 2g na 3g ili waweze kupata intaneti kwa urahisi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kondoa Dkt.Khamis Mkanachi akipitia mabanda mbalimbali ya maonesho ya nane nane katika viwanja vya nzuguni Jijini Dodoma amelisifia Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kuweza kuwa washindani katika ulimwengu wa kidigitali.

“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kuwezesha ushindani wa mashirika katika ulimwengu wa kimataifa.

” TTCL ilipokuwa imefikia na sasa ilipo ni hatua kubwa kwani hapo hawali shirika hilo lilikuwa katika haki mbaya lakini kwa sasa linaweza kuingia katika ushindani zaidi katika soko la kimataifa”ameeleza Mkuu wa Wilaya Kondoa.