Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
HIFADHI ya Taifa Kisiwa Cha Saanane, iliyopo mkoani Mwanza, imeshiriki mbio za Marathon zilizofanyika katika jiji hilo Julai 07, .2024, kwa lengo la kukuza Utalii wa ndani.
Akizungumza katika mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa rai kwa washiriki kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii kwa kutembelea vivutio vya Utalii ndani ya Mkoa huo ikiwemo Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane , Bismarck rock na vivutio vingine.
“Huu ni mwanzo mzuri wa ushiriki wa Marathoni katika Hifadhi. Hivyo, maandalizi ya marathon zinazokuja au zinazoendelea zilenge kupanua wigo wa kujitangaza zaidi haswa kupitia katika matukio kama haya,” amesema Said Mtanda.
Naye, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ambaye pia Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Saanane, Tutindaga George amefurahishwa sana na muitikio mkubwa wa washiriki waliojitokeza katika mbio hizo, ambapo kupitia Hifadhi wameweza kutangaza Utalii.
“Nawashukuru sana washiriki wote kwa kujitokeza. Niwasihi muwe mabalozi wetu wazuri kuitangaza Saanane na Hifadhi zingine za Taifa, na kila kunapokuwa na matukio ya kutangaza Utalii mjitokeze kwa wingi ili kuunga mkono jitihada za Rais katika kutangaza Utalii”.
Mbio za Transec Lake Victoria Marathon, zimewakutanisha wanamichezo wengi walioshiriki mbio za Kilometa 2.5, 5, 10, 21 na 42, wengi wao wakitokea katika Mkoa wa Mwanza pamoja na mikoa jirani huku ikiunganisha wanamichezo wengine kutoka mataifa ya kigeni.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru