Na Lubango Mleka, Timesmajira online – Tabora
JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa kituo cha Polisi Wilaya ya Igunga mkoani humo,WP. 8033 PC Victoria kwa tuhuma za kosa la uzembe wa kushindwa kuchukua hatua za usalama kwa wananchi na kushiriki kukinga mafuta kwenye gari lililopata ajali katika kijiji cha Igogo Kata ya Igunga.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mkoani hapa, juu ya tukio hilo la ajali iliyohusisha magari ya matatu ya mizigo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao,amesema Askari huyo. anatuhumiwa kushiriki kumpa mwananchi dumu kwa ajili ya kukinga mafuta kwenye ajali iliotokea Machi 28,2025 katika kijiji cha Igogo Kata ya Igunga mkoani Tabora.

Abwao amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Scania Tenka lenye namba za usajili T. 275 EK lenye tela namba T. 944 NZ lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Nzega, kuligonga gari aina ya Scania lenye namba T. 39 DUK lenye tela namba 302 DWD,lililokuwa linatokea Kagera kwenda Moshi na likiwa limebeba mahindi likiendeshwa na dereva Christopher Msoso,
Ambalo lilipoteza mwelekeo na kugonga gari jingine lenye namba T. 195 BSC Scania lenye tela namba T. DRW likitokea Congo kwenda Da es Salaam ambalo lilikuwa halina mzigo.

” Katika ajali hiyo mtu mmoja aliyefamika kwa jina la Nassoro Ally alijeruhiwa na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Igunga kwa matibabu zaidi na tunamshikiria dereva wa gari lililosababisha ajali na kuharibu mali,” amesema Abwao.

More Stories
Rais Samia atoa msaada kwa kituo kinachohifadhi wasichana waliokimbia ukatili
Mo Dewji na Urithi anaoujenga ,unavyoenda mbali zaidi ya mafanikio binafsi
Mulika Community kusaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili