Na Ashura Jumapili, Timesmajira Online,Bukoba,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA )Mkoa wa Kagera imeadhimisha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa msaada wa vitu mbalimbali na fedha taslimu vyenye thamani ya milioni 8 kwa kituo cha watoto yatima Ntoma kilichopo Bukoba Vijijini mkoani Kagera .
Naibu Mkurugenzi wa Fedha za makusanyo ya kodi na yasiyo ya kodi Ramadhan Sengati kutoka Makao Makuu ya TRA akizungumza wakati akikabidhi msaada huo amesema wameguswa na jambo la kuwanyonyesha watoto linalofanywa na kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kiluthel Tanzania (KKKT ).
Sengati,amesema TRA kama sehemu ya jamii kupitia wiki maalum ya kumshukuru mlipa kodi huwa wanafanya mambo mengi ikiwemo kupata wahitaji ambao wapo katika mazingira magumu ili waweze kuwachangia kwa kile walichojaliwa hivyo kwa mwaka huu wamechagua kituo cha watoto wadogo cha Ntoma.
‘’Tulichagua kituo hiki cha Ntoma kutokana na kazi kubwa ya walezi ya watoto hao ya mitume na manabii,sisi kama jamii pia tumeguswa na yanayotendeka hapa kituoni ,“amesema Sengati.
Amesema msaada uliotelewa ni vyakula ,vinywaji,viburudisho,sabuni,maziwa ya kopo na pampers vyote vinathamani ya milioni 7 na fedha tasilimu kiasi cha milioni 1.
Awali Msimamizi wa kituo cha Ntoma Sr.Peninnah Kaimukilwa,amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1952 na kina watumishi 17 walioajiriwa pia kinapokea watoto kuanzia mwaka sifuri hadi miaka miwili huku tangu kuanzishwa kumeisha huduma watoto 1317 hadi sasa.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ilikuwa ni kuwasaidia watoto waliopeza mama na wanaotelekezwa mitaani.
Pia amesema kituo hicho kinauwezo wa kuhudumia watoto 30 ila kutokana na changamoto mbalimbali za jamii ikiwemo vifo na watoto kutelekezwa kituo hicho kina watoto 42.
‘’Kituo hicho kimelazimika kuwa na idadi kubwa ya watoto kuliko uwezo wake kutokana na changamoto kuongezeka katika jamii kwa vile wazazi kufariki, kuugua afya ya akili ,kutelekeza watoto kwenye vituo vya afya na mitaani hasa maeneo ya mijini, “amesema Sr.Kaimukilwa.
Aidha amesema kituo hicho kina watoto wa kiume 24 na wakike 18 ambao jumla yao ni 42 kati yao waliotelekezwa ni 9.
Mchungaji Dkt.Paschal Matungwa Mkuu wa kitengo cha Diakoma KKKT ,ameishukuru TRA kwa kuguswa na watoto hao wenye uhitaji kwa kufika kuwanyonyesha ambao hawakupata bahati ya kunyonya maziwa ya mama zao kwa sababu mbalimbali.
Amesema mtoto mmoja kwa siku anakunywa maziwa ya kopo moja la lactogen hivyo uhutaji ni mkubwa kwa watoto huku miaka ya nyuma walikuwa wakipata misaada kutoka nje ya nchi kwa sasa wamesitisha huduma hiyo na kuwataka wajiendeshe wenyewe.
Hata hivyo wanaishukuru jamii kwa kuona umuhimu wa kuwahudumia watoto hao kwa kutoa misaada mbalimbali.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi