December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwahamasisha vijana ambao hawana ajira kuhudhuria kongamano la vijana litakalofanyika Mloo, mkoani Songwe kesho, likilenga kuwasaidia vijana kupata fursa ya kuwekeza na kufanya biashara na kujiajiri. Na mpiga picha wetu.

TPSF kushiriki kongamano la kuibua fursa za kiuchumi

a Mwandishi Wetu

TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inatarajiwa kushiriki kwenye
kongamano la siku moja mkoani Songwe linalolenga kuwaeleza vijana
fursa za kiuchumi mkoani mwao na Tanzania kwa jumla.

Akizungumzi ushirki na maandalizi ya kongamano hilo Jijini hapa jana,
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, amewambia waandishi
wa habari kwamba moja ya shabaha kuu za TPSF ni kuhakikisha sekta
binafsi ya siku za baadaye inajengwa na vijana wabunifu, wanye
kujituma sana na wenye kufanyakazi zenye tija.

“Kama sehemu ya mikakati yetu ya miaka mitano, TPSF kwa kushikiriana
na wenzetu wa Mkoa wa Songwe, tumeandaa kongamano la vijana ambalo
litafanyika Jumamosi ijayo.

Katika kongamano hilo fursa mbalimbali zitaoneshwa na namna vijana wanavyoweza kuwa sehemu muhimu katika ukuaji wa sekta isiyo rasmi hapa nchini,” amesema Simbeye.

Ametoa wito kwa vijana wa Mkoa wa Songwe kuhudhuria kongamono hilo
ili kupata ufafanuzi na maelezo juu ya fursa zilizomo mkoani mwao na
ambazo zitawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Amesema suala la kuikuza sekta binafsi na kuleta tija katika ukuaji wa
uchumi nchini linahitaji ushirikiano wa taasisi binafsi na za umma na
wadau wa maendeleo.

“Kazi yetu ni kuratibu shughuli za uchumi na uwekezaji hapa nchini.
Tunao vijana wengi ambao hawajanufaika na fursa kwenye mfumo wa uchumi
wetu usio rasmi. Tunaupongeza Mkoa wa Songwe kwa namna ambavyo
umewakumbuka vijana na kama sehemu ya mkakati wetu.

Tunaiomba mikoa, idara na taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao,” amesema.

Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yatategemea ni namna gani vijana
wanahusishwa katika kutumia fursa zilizomo katika kilimo, viwanda,
uvuvi, biashara na uwekezaji.

“Vijana ni rasimali muhimu katika ukuaji wa uchumi wa taifa lolote.
Hivyo Serikali na taasisi binafsi zinapotengeneza mipango na mikakati
yake lazima kuangalia nafasi ya ushiriki wa vijana,” amesema na
kuongezaka kuwa wanafarijika kuona mpango wao wa miaka mitano unaendelea vizuri.

“Tunapoelekea uchumi wa viwanda ifikapo 2025 kama ilivyoazimiwa na
Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John
Magufuli, ni lazima kuwaunganisha vijana na fursa za kimaendeleo
zilizopo hapa nchini. Kinyume na hivyo itakuwa kazi ngumu,’’
amesisitiza Simbeye.

TPSF ni taasisi ya kileleni inayounganisha vyama na jumuiya za sekta
binafsi na ni sehemu ya Baraza la Taifa la Biashara ambalo mwenyiti
wake wa taifa ni rais wa Tanzania.