January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPHPA:Wananchi toeni taarifa za wadudu waharibifu shambani

Picha ya kwanza (nzige) na ya pili (kweleakeelea) ) zinaonesha visumbufu vya mazao vinavyoshambulia mazao shambani

Na Joyce Kasiki Timesmajira online,Dodoma

MAMLAKA ya Mimea na Viuatilifu nchini (TPHPA) imewaasa wananchi kujenga desturi ya kutoa taarifa mapema,mara tu wanapoona ndege au wadudu waharibifu ( visumbufu vya mazao) wameingia shambani ili hatua za kuwadhibiti zichukuliwe haraka kabla ya kufanya uharibu wa chakula.

Godlove Kirimbo kutoka TPHPA ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda hilo kwebye maonesho ya wakulima na wafugaji 88 yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema ,wananchi wanapoona visumbufu hivyo ,watoe taarifa kwa halmashauri husika ambayo pia itatoa taarifa kwenye Mamlaka hiyo kisha hatua za kuwadhibiti zinafuata .

Amesema vipo visumbufu vya mlipuko ni pamoja na ndege aina ya kweleakwelea ,panya waharibufu wa mazao,nzige na viuavijeshi huku akisema ni visumbufu vya mlipuko kwa sababu hutokea kwa ghafla vikiwa katika makundi makubwa na kusababisha uharibifu wa chakula ndani ya muda mfupi.

Kirimbo amesema kuanzia februari mwaka huu, kulikuwa na mlipuko mkubwa wa kweleakwelea kwenye halmashauri 24 nchini ambapo zaidi ya kweleakwelea milioni 70 walivamia na kushambulia mazao ya nafaka mtama,uwele,mpunga na alizeti.

“Mwaka huu tumerekodi kweleakwelea zaidi ya milioni 70 walikuwa Tanzania na kundi sogo la kweleakwelea lenye milioni moja linaweza kuharibu tani 25 kwa siku moja,

“Lakini kundi dogo la nzige milioni 40 linaweza kuharibu chakula ambacho kingeweza kulowa na watu 35,000 kwa siku,kwa hiyo unaona kwamba viumbe hivi wakiachwa ,nchi itaingia kwenye baa kubwa la njaa.

Amesema , visumbufu vya mlipuko ni visumbufu ambavyo ni hatari kwa usalama wa chakula nchini huku akisema TPHPA wana jukumu la kuhakikisha usalama wa chakula nchini unalindwa kwa kuvidhibiti visumbufu hivyo.

Kwa mujibu wa Kirimbo,visumbufu aina ya kweleakwelea ni hatari kwa usalama wa chakula kwa sababu wana tabia kubwa mbili ikiwemo kuishi kwenye makundi makubwa ya kuanzia milioni moja kuendelea