Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
MTANDAO wa Polisi Wanawake wilayani Nkasi mkoani Rukwa (TPF-Net),imeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuwatembelea wagonjwa hospitali ya Wilaya Nkasi na kutoa zawadi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwa wagonjwa Mwenyekiti wa TPF-Net wilayani Nkasi,Ivona Mwanga, amesema mtandao huo umeundwa kwa ajili ya kuisaidia jamii kukabiliana na vitendo mbalimbali vya ukatili.

Hivyo ameitaka jamii kutokaa kimya pale wanapoona wanaonewa bali wakimbilie Polisi ambako lipo dawati la jinsia na Watoto ambako wanaweza kupata haki zao za msingi.
Katibu wa mtandao huo,Anna kisimba kwa upande wake ameitumia siku hiyo kutoa elimu kwa jamii na kutaka kulitumia dawati la jinsia la jeshi la Polisi katika kudai haki zao za msingi.
Amedai kuwa wao kama Polisi Wanawake wamejikita kuhakikisha makundi mbalimbali katika jamii yanapata haki sawa bila ya kujali jinsia ili jamii inaishi kwa amani na utulivu.
Mkuu wa kituo cha Polisi Namanyere,Francis Mabisi amesema,wameamua kuadhimisha siku hiyo ya wanawake kwa kumtembelea wagonjwa na kuwapatia misaada,ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma za kipolisi kwa jamii na kujenga uhusiano.
Ofisa ustawi wa jamii Hospitali ya Wilaya ya Nkasi Jackson Bolingo, amewashukuru Polisi hao kwa kuwatembelea wagonjwa hospitalini hapo huki akiahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi katika kukabiliana na vitendo mbalimbali vya uhalifu.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani mwaka huu yamebeba ujumbe mahususi usemao : Wanawake na Wasichana 2025 Tuimarishe haki,Usawa na Uwezeshaji.

More Stories
Nachingwea waanza kuona manufaa vituo vya kudhibiti wanyamapori waharibifu
Ajuza aileza timu ya msaada wa kisheria anavyonyang’anywa urithi kisa kuzaa watoto wa kike
DC Mpogolo awataka wenyeviti wa mitaa kusimamia usafi