Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline, Dar
KAMPUNI Ya TotalEnergies Marketing Tanzania imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maboresho sekta ya elimu, na katika kuunga mkono juhudi hizo, imezindua programu ya ‘Via Road Safety’ mahususi kwa ajili ya usalama barabarani kwa wanafunzi huku ikielekezwa kuwa elimu hiyo iende sambamba na usalama wao kijinai kwa kuhakikisha wanafunzi hawarubuniwi na yeyote pindi wanapotumia barabara.
Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Mamadou Ngom aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania, Getrude Mpangile katika hafla fupi iliyofanyika jana, shule ya msingi ya Makuburi, iliyopo wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mpangile alisema, kufuatia kazi nzuri ya serikali ya awamu ya 6 kwenye maboresho ya elimu nchini, kampuni yake ya TotlEnergies, inaunga mkono kwa mradi ili kupunguza madhara ya ajali za barabarani zinazohusisha watoto na kuwaacha na madhara ya kudumu ikiwemo ulemavu hali inayokwamisha kutimiza ndoto zao katika elimu.
“Kutokana na sababu hizo TotalEnergies Foundation kwa kushirikiana na TotalEnergies Marketing Tanzania tulianzisha mradi huu wa elimu ya usalama barabarani unaotambulika kama ‘Via Road Safety’ ili kuchangia katika kupunguza madhara yanayotokana na ajali za barabarani kwa kuwaelimisha watoto wetu kutumia barabara kwa uangalifu na kufuata kanuni na sheria.” Alisema.
Getrude alisema, Mpaka sasa watoto zaidi ya elfukumi na sita, wamenufaika na mradi huo tangu ulipoanza na kwa mwaka huu wanatarajia kuwafikia watoto elfu sita katika shule sita za Mkoa wa Dar es Salaam.
” Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuhakaikisha usalama barabarani unazingatiwa hususani kwa watoto tunaunga mkono jitihada hizo. Mradi huu pia unatarajiwa kuanzisha klabu za mabalozi wa usalama barabarani na mwaka huu tunatarajia kupata mabalozi 120 wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nne ambao watasaidia mradi huo kuwa endelevu kwa kuwafundisha wenzao na kufanya elimu hiyo kuwa endelevu.” Ameeleza.
Aidha alisema, Mradi huo utatoa fursa ya elimu kwa wanafunzi za Msingi za Umma na kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Nafasi Art Space ambao wamekuwa wakiwafundisha watoto juu ya usalama barabarani kupitia ubunifu wa nyimbo, mashairi na maigizo ambayo yamekuwa yakipeleka ujumbe kwa ufanisi zaidi kwa wanafunzi hao.
Mpangile amesema; Uzinduzi wa mradi huo na mashindano kupitia ‘Via Road Safety’ kwa msimu huu wa tatu: katika mashindano ambayo washindi hupata zawadi mbalimbali na fursa ya kushiriki mashindano Barani Afrika na baadaye Ulimwenguni kwa mwaka huu kipekee zaidi mshindi atapata zawadi ya kutatuliwa tatizo lililooneshwa.
“Kwa miaka hii tuliyofanya mradi huu watoto wamekuwa wakiibua matatizo mbalimbali kuhusiana na Usalama barabarani…shule hii ya Makuburi mwaka jana walionesha changamoto ya kutokuwepo kwa ukuta kwenye sehemu ya shule hali iliyopelekea usalama finyu kutokana na pikipiki kukatiza katika maeneo ya shule kwa mwaka huu mshindi atapatiwa fedha ya kutatua changamoto aliyoionesha.” Alisema.Na Mwandishi Wetu
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
.
More Stories
Uokoaji Kariakoo ni ushuhuda wa Utanzania
DC Ileje awafunda wanufaika TASAF
DC Mgomi: Mtakaohitimu TASAF endeleeni kubaki kwenye vikundi