January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Total yaadhimisha Valentine ikihimiza upendo, yazawadia wateja

Na Reuben Kagaruki, TimesMajira Online, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania, imeungana na Watanzania kusherehekea sikukuu ya wapendanao ya Valentine kwa kutoa zawadi ya ua kwa kila mteja aliyefikala kuweka mafuta katika baadhi ya vituo cha Total nchini kote kama ishara ya upend.

Sikukuu hiyo imeadhimishwa duniani kote leo,ambapo Kampuni hiyo imetumia fursa hiyo kuhamasisha upendo miongoni mwa Watanzania.

Akizungumzia kuhamasisha upendo, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Total, Getrude Mpangile, amesema kampuni ya TotalEnergies inawapenda Watanzania na ina upendo siku zote ndio maana inawaletea mafuta bora yenye kiambata cha excellium na bidhaa bora za vilainishi.

“Na leo ndio imeungana na Watanzania kuwaonesha upendo kwa kuwapatia zawadi ya sikukuu ya Wapendanao ya Valentine kwa wateja wao, kwa kuonesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya Valentine kwa upendo,”alisema Mpangile.

Mpangile amesema Total imeamua kuwahamasisha Watanzania kuwa na upendo kwa kupendana kama TotalEnergies inavyowapenda Watanzania, na amewakumbusha Watanzania, kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha Total, haujazi mafuta tu, bali unajaza mafuta ya Excellium.

Amesema ni mafuta yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo, kwa kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo, yakiboresha injini ya gari yako.

TotalEnergies ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ni ni moja ya makapini ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote.

Ina wafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.

Kuhusu Total

TotalEnergies imeanzisha kampeni kabambe utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae.

TotalEnergies imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara hili la Afika kujiletea maendeleo.

Mbali na hilo. Kampuni ya TotalEnergies ndio wasambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami, na GPL, nk) katika bara la Afrika.

Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanya biashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikana wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu – kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua.

Biashara ya TotalEnergies Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo.

Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya TotalEnergies ” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya TotalEnergies.

Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya TotalEnergies Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa AWANGO kwa jamii ya Watanzania.