January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tobiproduct kuja kivingine maonesho ya sabasaba Dar

Na David John ,Timesmajiraonline

MKURUGENZI wa Kampuni inayozalisha bidhaa zitokanazo na karanga ya Seasoning Palet Tobiproduct, Agatha Laizer amesema maonesho ya sabasaba yanatoa fursa kwao kama wajasiliamali kuweza Kujitangaza na kupata fursa kuonesha kazi nzuri zinazofanywa na watanzania.

Amesema kuwa maonesho hayo ya kimataifa ya sabasaba ambayo yanafanyikia Kila mwaka hapa nchini yanawafanya wafanyabiashara kupiga hatua kwa kutumia majukwaa tofauti ambayo wanashiriki.

Agatha ameyasema haya leo Mei 19,2023 katika viwanja vya maonesho ya sabasaba vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya kilwa wakati akizungumzia maandalizi ya maonyesho hayo ya sabasaba yanayotarajia kuaza Juni 28 na kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.

“Niwatie moyo wafanyabiashara wenzangu hasa wale wenye biashara ndogo ndogo katika maonyesho ya mwaka huu ya sabasaba tuyatimie vilivyo ili kuendelea kutengeneza matandao na Kujitangaza zaidi.amesema Agatha

Nakuongeza kuwa “tutakaposhiriki mwaka huu katika maonesho haya tutakuwa na uwezo wa kufanyakazi zaidi na kutengeneza mtandao mkubwa wa biashara ili kupata fursa mbalimbali zitakazotufanya tuzidi kuendelea mbele zaidi,”amesisitiza

Aidha ameishukuru TanTrade kwa kuanza maandalizi ya maonesho ya Sabasaba mapema hivyo amewataka wakinamama, vijana wasibaki nyuma kushiriki kwani anatambua kuwa wanabidhaa nzuri zenye ubora ambazo zinaweza kushindana na masoko mbalimbali ya nje ya nchi.

“Nawashukuru sana TanTrade Kwa kutushirikisha katika maandalizi kwaniaba ya wajasiliamali wengine hivyo ni Imani yangu kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali wengi watapata fursa ya kushiriki kikamilifu kwenye maonesho ya mwaka huu,”amesema.

Pamoja na hayo amesema yeye kama mkurugenzi wa Kampuni ya palet Tobi product wamejipanga vizuri kwalengo la kuwaletea kitu kilicho Bora kupitia maonesho ya kimaitafa ya sabasaba ambapo kwamujibu wa TanTrade kutakuwa washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi na ndani ya Tanzania.