December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMX kuimarisha mifumo ya utendaji kazi

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Soko la bidhaa Tanzania (TMX ) limebainisha kuwa litaendelea kuimarisha mifumo iliyopo katika utendaji kazi wa taasisi hiyo, ikiwemo mfumo wa stakabadhi za ghala, na ushiriki wa vikundi vya wakulima pamoja na kutoa elimu ili kuwafikia wadau wengi na hivyo kuongeza mchango wake katika uchumi wa nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa TMX Godfrey Malekano katika mkutano kati ya wahariri na waandishi wa vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar Es SAlam ambapo alisema kazi ya kujenga mfumo imara wa soko la bidhaa inategemea mchango wa serikali taasisi na sekta binafsi hivyo ushirikiano ni muhimu kufikia Adhma hiyo.

Aidha amesema kuwa kwa sasa soko hilo linafanya mauzo ya papo kwa papo huku lengo likiwa ni kuanzisha mauzo ya mkataba pale miundombinu itakabobpreshwa na kuongeza kuwa soko hilo linasaidia taarifa za ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa utoaji wa vibali kwa usafirishaji wa bidhaa pamoja na upatikanaji wa fedha za kigeni.

Pia amesema kutokana na kuipa kipaumbele Sera ya soko la pamoja la Afrika hivyo ni muhimu kuzingatia viwango vinavyofanana ili kuweza kuboresha biashara kati ya nchi na nchi ndani ya Afrika.

Aidha amesema juhudi zilizofanyika Hadi sasa ni kuendelea kuendelea kuboresha mfumo wa kielektroniki ili kuongeza bidhaa zaidi kwaajili ya mauzo. 

Pia amesema kwa sasa mfumo wa kielektroniki wa TMX unaweza kuhusisha ‘reverse actions’ ambapo wanunuzi wanaweza kutangaza kununua kiasi Fulani Cha bidhaa ya daraja maalum katika eneo maalumu la kuwasilisha na wauzaji kushindana kwa bei kwenye mfumo wakati wa mauzo.

Kuhusu faida ya soko kwa upande wa serikali Malekano amesema ” Ni njia rahisi ya kukusanya mapato kwa Halmashauri, upatikanaji wa taarifa za kuaminika,ni njia rahisi ya ukusanyaji mapato ya Taasisi husika, urahisi wa usimamizi wa utoaji wa vibali husika kwa usafirishaji wa bidhaa zilizouzwa”

“Muda zaidi kwa wadau wengine kujikita katika kuboresha uzalishaji wa mazao, Kuhamasisha kampeni ya uchumi wa viwanda, kusaidia upatikanaji wa fedha za kigeni, na kusaidia biashara ya Kimataifa kwa gharama nafuu (AFCFTA)”

Faida za soko la bidhaa Tanzania kwa upande wa mteja, Malekano amesema mnunuzi atakua na uwezo wa kupata mazao mengi na yenye ubora kwa wakati mmoja, kupunguza gharama (muda na fedha), kupunguza athari mbalimbali yaani kwenye ubora na wizi, upatikanaji wa taarifa za soko, na kujikinga na mabadiliko hasi ya bei.

Kwa upande wa mkulima au muuzaji, atanufaika na soko hilo kwa kuimarisha bei ya soko, upatikanaji wa taarifa za soko, kuongeza kwa ufahamu wa uzalishaji Bora, uhakika wa malipo, na mkulima kuwa huru kuamua bei aliyoridhia bidhaa zao.

Akizungumza kwa niaba ya jukwaa la wahariri (TEF ) Jackton Manyerere amewashauri TMX kutumia vyombo vya habari Ipasavyo kuelezea kazi wanazofanya kwa kina ili kuwezesha wananchi kuelewa zaidi fursa zinazopatikana ndani ya soko hilo la bidhaa Tanzania.