December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMDA yateketeza bidhaa bandia zenye thamani ya shilingi bilioni 35.5 mwaka 2021/22

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA),Adam Fimbo amesema kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 imekamata dawa,vifaa tiba na vitendanishi ambavyo havijasajiliwa vyenye thamani ya shilingi  bilioni 35.3.

Fimbo amesema hayo Jijini hapa leo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo Kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 na matarajio kwa mwaka 2021/2023 ambapo amesema TMDA iliendesha operasheni tatu maalum kwa mikoa 14 ambapo maeneo 1,355 ya biashara nafanya bidhaa bandia katika soko kupungua hadi  kufikia asilimia moja.

“Ili kulinda afya za walaji, TMDA imekuwa ikifuatilia,kuondoa na kuteketeza  bidhaa ambazo hazikidhi vigezo vya ubora,usalama na ufanisi ili kuepusha zisitumiwe na kwamba mpango wa ufuatiliaji wa ubora wa bidhaa katika soko hutumika wakati wa ufuatiliaji huo,”amesema.

Ameeleza kuwa katika ufuatiliaji huo,jumla ya sampuli za dawa 215 zilichunguzwa ambapo matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa dawa zote sawa na asilimia 100 zilifaulu vipimo vya kimaabara.

“Kwa upande wa vifaa tiba na vitendanishi,jumla ya sampuli za matoleo 567 zilichunguzwa na sampuli 522 sawa na asilimia 92 zilikidhi vigezo,hiki ni kiashiria kuwa kiasi kikubwa cha bidhaa za dawa na vifaa tiba kilichoko sokoni kinaidhi vigezo vya ubora,”amesema

Pamoja na hayo alifafanua kuwa katika kuteketeza bidhaa zisizofaa Kwa matumizi, katika mwaka wa fedha 2020/2021 kiasi na thamani ya bidhaa za dawa na vifaa tiba visivyofaa zilizoteketezwa imeongezeka kutoka tani 14,704.80 zenye thamani ya shilingi bilioni 8.5 hadi kufikia tani elfu 35,547.47 zenye thamani ya bilioni 35.53 ambazo ziliteketezwa kwa mwaka 2021/22.

“Bidhaa hizi zinajumuisha bidhaa zilizotolewa taarifa na zile zilizokamatwa katika kaguzi mbalimbali  ambapo kuongezeka kwa bidhaa zilizoteketezwa Kutokana na kuimarisha ukaguzi na elimu kwa umma inayosaidia wateja kutoa taarifa juu ya bidhaa zisizofaa Kwa matumizi,”amesema

Aidha amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi juu ya ubora,ufanisi na usalama wa dawa,chanjo na vifaa tiba TMDA imeendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali katika mikoa 23 ikiwa ni pamoja na kuanzisha vilabu 55 vya masomo kwa baadhi ya Shule za sekondari .

Pia amesema wameanzisha vilabu kwa Shule za mikoa ya Dodoma, Dar Es Salaam, Pwani,Singida, Morogoro na Mtwara,vilevile kupitia mitandao ya kijamii idadi ya watu wanaofuatilia kurasa za mitandao husika imefikia 193,000.

Pamoja na kashiriki kwenye mipango ya uwianisho wa taratibu za udhibiti wa dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC)na Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika(SADC)ambapo kupitia mipango hiyo Taasisi za udhibiti wa dawa za nchi wanachama zimekuwa na mifumo thabiti ya pamoja .

“Hatua hii inasaidia upatikanaji wa dawa Bora ,salama na fanisi ambapo kupitia EAC hadi sasa jumla ya dawa 85 zimesajiliwa na sasa zinauzwa kwenye nchi zote wanachama,kupitia mashirikiano haya , mamlaka imeweza pia kutoa mafunzo kwa wenzetu wa mamlaka ya udhibiti wa dawa Botswana (BOMRA)na mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini Uganda (NDA),”amesema.