April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMDA yashinda tuzo za PRST ya Umahiri katika kampeni bora ya utoaji elimu jamii

Na Penina Malundo, Timesmajira 

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),imeshinda Tuzo ya utoaji elimu kwa jamii iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).

 Tuzo hiyo imezotolewa na PRST jana Machi 29,2025 jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na watu kutoka taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi.

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.

Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika na Taasisi mbalimbali ikiwa ni ishara nzuri ya maboresho yanayofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.