Na Mwandishi wetu, timesmajira,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekamata dawa ambazo hazijasajiliwa zenye thamani ya TSh 294,486,590 milioni ambapo tozo yake inakaribia kuwa Milioni 80 zimekamatwa kufuatia ukaguzi maalum, uliofanyika eneo la Mtaa wa Kitumbini katika Kata ya Mchafukoge katikakati ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika eneo la tukio, Meneja wa Kanda wa TMDA, Adonis Bitegeko amesema timu ya TMDA ya Kanda ya Mashariki, imekamata ghala bubu ambalo halijasajiliwa na TMDA, ambapo limebainika ghala hilo lipo chini ya mmiliki wake Amaiya Rijendra likiwa limehifadhi dawa mbalimbali za binadamu ambazo hazijasajiliwa.
Amesema walifanikiwa kuwasiliana na Jeshi la Polisi na kumchukua mtuhumiwa kwaajili ya hatua zaidi za kisheria na TMDA tumekusanya dawa zote ambazo hazijasajiliwa na kuzichukua.”Tumechukua taratibu za kuziorodhesha na hatua kadhaa za kisheria ikiwemo kuwatoza faini na pia watatakiwa kulipia gharama za kuziteketeza”,amesema
Aidha, TMDA ilitoa onyo kwa wanaoendelea kufanya biashara hiyo haramu kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo pia amewaonya pia wataalamu husika wanaojihusisha na biashara hizo haramu kuwa hawatosita kuwafutia leseni zao za kitaaluma.
Ametaja dawa hizo zilizokamatwa kuwa ni pamoja na Dawa za magonjwa ya shinikizo la damu, dawa za kutoa ujauzito na dawa nyingine tofautitofauti.
Mtuhumiwa aliyekutwa nazo ni mtanzania mwenye asili ya India ambapo alipohojiwa alikiri kuendesha ghala hilo bubu pasipo na kibari na kinyume na sheria kwa kile alichodai hakufahamu mamlaka husika za usajili,
More Stories
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500
TMA kuendelea kufuatilia mifumo yake
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi