Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
MKURUGENZI wa Huduma za Tabiri Mamlala ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt.Hamza Kabelwa amewakumbusha waandishi wa habari kuwa Mabalozi wazuri wa TMA na kuwa daraja kati ya Mamlaka hiyo na jamii katika kuelezea matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii.
Akizungumza leo Mkurugenzi huyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt.Agnes Kijazi wakati akifungua warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2022 nchini kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania.
Amesema taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa wananchi katika shughuli zao za kila siku wanahabari wanapaswa kuhakikisha taarifa za hali ya hewa za kila siku ikiwa ni pamoja na taarifa za hali mbaya ya hewa zinapata nafasi katika vyombo vyao vya habari
Dkt.Kabelwa amesema taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na athari zake ni muhimu kupatikana kwa wakati ili kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
Amesema TMA inamchango mkubwa katika ukuaji wa kiuchumi kwa vile huduma za hali ya hewa ni mtambuka na zinahitajika katika kila sekta.
“Mamlaka imeendelea kutoa taarifa za kila siku na tahadhari dhidi ya matukio ya hali mbaya ya hewa sambamba na kutoa huduma za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama vile usafiri wa anga, usafiri kwenye maji, usafiri wa nchi kavu, kilimo, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, ujenzi, maji, nishati, utalii, maafa, viwanda , afya, mazingira, mawasiliano, bima, Taasisi za kifedha na mengineyo kwa ajili ya usalama wa watu na mali zao”,Amesema
Amesema Mamlaka imeendelea kutoa taarifa kila siku na tahadhari dhidi ya matukio ya hali mbaya ya hewa Sambamba na kutoa huduma za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Ametaja sekta hizo ni pamoja na usafiri wa angani, usafiri wa kwenye maji,usafiri wa nchi kavu pamoja na Kilimo, Madini na Gesi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato