December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMA yatangaza msimu wa mvua za masika

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira, online

Mamlaka ya hali  ya hali ya hewa nchini TMA, imetangaza kuwa msimu wa mvua za masika kwa baadhi ya mikoa mingi  zinatarajiwa kunyesha za wastani hadi chini ya wastani huku mikoa michache ikipata  mvua za wastani  hadi juu ya wastani.

Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo katika Ofisi za TMA-Dar es Salaam, Ubungo Plaza, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a amesema maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani ni pamoja na Dar es salaam mkoa wa Pwani,Unguja na Morogoro kaskazini huku mikoa inayopata mvua A wastani hadi chini ya wastani ni pamoja na  na Kagera,Geita,Mwanza ,Shinyanga,Simiyu,Mara,Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Tanga pamoja Kisiwa cha Pemba.

Aidha, ameongezea kuwa Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei 2023, hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini

 Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Rose Senyangwa amesema mifumo ya hali ya hewa joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kati la bahari ya pasifiki, joto la wastani linatarajiwa katika eneo kubwa la kitropiki la bahari ya Hindi huku joto la juu ya wastani likitarajiwa katika eneo la Mashariki mwa Bahari ya Atlantiki hali hiyo itadhoofisha mifumo inayosababisha mvua.