Na David John, Timesmajira Online, Mbeya
MENEJA wa Huduma ya Hali ya Hewa Kilimo na Mamlaka Ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Isack Yonah Amesema Mamlaka ya hali ya hewa ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inafanya kazi Zanzibar na Tanzania Bara nakwamba kuna vituo Visiwani humo na kuna vituo pia Tanzania bara.
Amesema kuwa Mamlaka hiyo ni Taasisi iliyoazishwa kwa sheria namba 2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania na inaipa mamlaka hiyo kama mtoa huduma lakini pia kama mdhibiti na mratibu wa huduma zote za hali ya hewa nchini.
Meneja Yonah ameyasema haya Agosti 5 wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye viwanja vya maonyesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini mbeya ,ambapo amesema kuwa wamelazimika kushiriki maonyesho kama sehemu ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye maonyesho hayo ili kuona teknolojia mpya iliyotumika kutoa huduma za hali ya hewa.
Ameongeza kuwa wao kama Mamlaka wako tayari kujibu maswali ya wananchi kupitia maonyesho hayo ya nanenane lakini pamoja na hayo mamlaka hiyo ipo tayari kuwaelezea wananchi ninamna gani mchakato mzima utakavyotumika kutabili na pia kueleza kwamba kwakuwa sheria imetoa fursa kwa watu wote pengine wanatamani kufanya huduma wajisajili ili kuweza kupata huduma hizo za utabili.
Amesema kuwa vituo vyao vya hali ya hewa vinauwezo wakujua mvua itanyesha kiasi gani hivyo kwa mkulima kujua kiasi cha mvua itakayonyesha ni muhimu sana ,lakini pia Mamlaka inakifaa kingine ambacho kinatumika kupima nguvu ya jua limewaka kwa muda gani na lilikuwa na nguvu gani ambayo ni muhimu sana kwa kilimo kwasababu mazao yanategemea joto kwani joto likiwa nyuzi joto kumi ukipanda mazao hayawezi kuota hata ukuaji wake unachelewa ndio maana maeneo kama Mbeya mazao yanachukua muda mrefu.
Amesema nivizuri watu kujua kwamba taarifa za hali ya hewa zinatumika kwa mazingira gani lakini kuna chombo kingine ambacho kinapima upepo ambacho kina sensa na mawimbi yanaonyesha upepo unatoka wapi na unaelekea wapi kwahiyo huduma za hali ya hewa zinaendelea kuwa bora na bora.
Meneja Yonah ameongeza kuwa nimuhimu sana sana vituo vya Mamlaka ya hali ya hewa hasa kwa wanaoazisha kuhakikisha kwamba vituo vyao vinasajiliwa na ili viweze kwenda sawa na malengo ya mamlaka husika mdhibiti na wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kwahiyo chombo hicho sio kama kile cha zamani ambacho kilikuwa kinatunza kipima joto lakini sasa hivi ni vya kisasa.
“Taarifa hizi zote zinachakatwa kwenye mtambo huu na unahakikisha kwamba unasoma na kuonyesha namba ili kujua imesoma kwa namna gani na taarifa hizi zinasaidia kutabiri.mfano kwenye maeneo haya ya viwanja vya maonyesho inaonyesha kesho kuazia saa tatu usiku wa leo hakutarajii kuwa na mvua na upepo unatarajia kuvuma kutoka kusini mashariki lakini hali ya ubaridi inatarajia kuongezeka kidogo kuliko leo nyuzi joto kama saba katika maeneo haya tofauti ya leo kulikuwa nyuzi joto kama tisa hivyo kutakuwa na hali ya baridi kuamkia kesho.”amesema
Ameongeza kuwa utabiri huo mara nyingi unakwenda mpaka saa sita usiku na baadae wanatoa utabiri mwingine ilikuhakikisha wananchi wa maeneo husika kila siku wanaendele kupata utabiri lakini pia kuna wadau mbalimbali kama watu wa ujenzi wa barabara na magonjwa mbalimbali zinahitajika taarifa za hali ya hewa kwani ni muhimu sana pamoja na watu wa madini na wale wanaofanya miradi mikubwa ya kitaifa wanatarajia taarifa zao za hali ya hewa nahiyo nikwasababu kabla hujafungua shamba lazima kupata taarifa za mamlaka hiyo.
Menaja huyo amesema kuwa taarifa hizo zote zinachakatwa lakini hawatumii taarifa zao tu lakini wanataarifa zingine kutoka mtandao wa kimatifa ndio maana nchi ili iweze kufika kwenye viwango vya juu kuna rada ambazo zinasaoidia kupata mtabiri wa muda mfupi wa saa kama mbili ,na nchi imewekeza kwenye rada na zipo rada tatu ipo Dar es saalam, Mwanza Mtwara ,na nyingine zitakazokuja zitakuwa Mbeya kigoma ,kilimanjaro na kigoma na taarifa hizo ni muhimu sana hivyo watu wanaalikwa ili kupata taarifa ya hali ya hewa ambayo nimuhimu sana.
More Stories
Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa Kimataifa matumizi bora ya Nishati
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa