May 30, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TLP yamchagua Rwamugira kugombea Urais

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar

CHAMA cha Tanzania Labour Party (TLP) kimemchagua Yustas Rwamugira, kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika  wilaya Ubungo mkoa Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa chama cha cha hicho jijini hapa leo,Mei 26,2025 Mwenyekiti wa uchaguzi huo Coaster Jimmy, amesema jumla ya wapiga kura 102 na  waliopigiwa kura walikuwa watatu,Neema Nyerere alipata kura 6 ,Wilson Ella’s 46 na Yusuph Wangira amepata kura 50 hivyo chama hicho kimemtangaza Yusuph Wangira ndiyo atakaye kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  TLP .

Akishukuru wanachama katika uchaguzi huo Rwamugira amesema anawakikishia ushindi wa chama chao katika uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani mikoa yote na mgombea mweza wake Amana Selemani Mzee.

Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa vyama vya Siasa Tanzania Sisty Nyahoza ,amewapongeza Tanzania Labour Party TLP, kwa kufanya uchaguzi kwa amani wa chama hicho .

Msajili Nyahoza amesema katika uchaguzi lazima ukubali mambo mawili kushinda na kushindwa na uchaguzi wenu umeenda vizuri Demokrasia imefanya kazi hivyo aliwaomba wawe wamoja kama chama wafanye kazi za chama na kuwa wastamilivu aliwapongeza walioshinda na walishindwa.

Amesema vyama vitakavyoshiriki uchaguzi mwaka huu 2025 mwezi Oktoba vipo 18 na yote vishiriki uchaguzi na kuwataka wadumishe amani.

Kwa upande wake mgombea urais wa Tanzania Labour Party TLP ambaye kura hazijatosha ameonesha kutoridhishwa kwa matokeo hayo ambapo amesema uchaguzi wa chama hicho siyo sahihi kwani amesema jumla ya Wapiga kura ni 170 huku akidai kati ya hao 13 ni Mamluki na ndiyo amedai wamesababishwa kushindwa kwake.