Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA, mwaka 2026 itakayoandaliwa na nchi za Marekani, Canada na Mexico itajumuisha timu 48 ambazo zitakagawanywa katika makundi 12 yenye timu nne tofauti.
Jumla ya michezo itakuwa 104 kutoka 64 ya michuano iliyopita. Timu mbili kwenye kila kundi zitasonga mbele huku zingine 8 bora zikivuka kama mshindi wa tatu.
Mbali na mabadiliko hayo mapya ya mfumo, kikao cha Baraza la FIFA kilichofanyika Machi 14 mwaka huu huko Kigali, Rwanda, FIFA imeainisha kuwa michuano hiyo ya Kombe la Dunia 2026, itaanza kutimua vumbi siku ya Jumapili, Julai 19, 2026.
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes