December 1, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo wazindua kampeni ya ‘CHA WOTE’ wateja kujishindia zawadi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi Maisha ya kidijitali, Tigo, leo imetangaza kuzindua kampeni mpya inayojulikana kama ChaWote ambapo wateja watajishindia zawadi kambabe pale wanapofanya miamala kwa kutumia mtandao wa Tigo. Hii ni promosheni ya kipekee kwani kila mteja wa Tigo ni mshindi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni iyo Bi. Angelica Pesha Afisa Mkuu wa Tigo Pesa amesema

” Kampeni hii inawapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi za fedha taslimu hadi TShs 5, 000, 0000 na bonasi za papo hapo za hadi dakika 100 na SMS 100 kwa siku 90 , Ili kuweza kuwa mshindi kwenye kampeni hii ya ChaWote, wateja wa Tigo wajinunulie vifurushi vyao pendwa vya siku, wiki na mwezi kupitia Tigo Pesa kwa kupiga 15001# au Tigo Pesa App. Pia wateja wanapolipia huduma au bidhaa kupitia Lipa kwa Simu watapa bonus za papo hapo za Dakika na SMS na kuingia kwenye droo inayowapa nafasi ya kujishindia hadi TSh 1,000,000 kila siku na TSh 5,000,000 kila mwezi “.