January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo wakutana na wateja wake, wasikiliza changamoto wanazokabiliana nazo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya simu za mikononi tigo imewakutanisha wateja wake wanaotumia mtandao wa tigo kufanya biashara mbalimbali kanda ya kaskazini kwa kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo na kutoa elimu kwa huduma mpya zinazotolewa na kampuni hiyo.

Wakionge mjini moshi katika halfa ya kuwakutanisha wateja wa tigo kanda ya kaskazini maafisa wakuu wa tigo pesa Anjelika Presha na John Silima wamesema kuwakutanisha wafanyabiashara hao ni moja ya kutoa fursa yakuweza kupanua biashara zao kwa kutumia huduma mbalimbali za tigo pesa.

Wamesema tigo business ipo kuboresha biashara mbalimbali za watu zikiwemo biashara kubwa,za kati na biashara ndogo pamoja na kusaidia katika nyanja za masawaliano.

Nao baadhi ya wafanyabiashara kanda ya kaskazini wameipongeza tigo kwa kazi nzuri wanazozifanya katika utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za tigo pesa,mawasaliano pamoja na sehemu ya faida wanazorudisha kusaidia jamii.