Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
Tigo Tanzania yakabidhiwa rasmi tuzo ya Mtandao Wenye Kasi zaidi Tanzania kwa mwaka wa 2023 iliyotolewa na taasisi ya Kimataifa ya Ookla.
Ookla ni taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa huduma za intaneti duniani,ikiwemo speed/kasi ya intaneti na muda wa kupakua au kupakia maudhui mtandaoni.
Tuzo hii ni matunda ya uwekezeji unaoendelea kufanywa na Tigo Tanzania ili kuboresha miundombinu ya mtandao . Kama mnavyofahamu mwaka 2022 Tigo Tanzania ilianza kutekeleza mpango wa miaka mitano unaolenga kuwekeza kiasi cha shilingi za kitanzania zaidi ya Trilioni moja kwenye miundombinu ya mtandao wetu.
Uwekezaji huu pia, ni moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Axian Telecom Group, inayomiliki kampuni ya Tigo Tanzania.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua