Na Jackline Martin, TimesMajira Updates
KWA kipindi cha mwaka wa fedha Julai 2023 hadi Juni 2024, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi 707 ukilinganisha na miradi 369 iliyosajiliwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022|2023 .
Miradi hiyo ya 2023/2024 ina thamani ya dola za Marekani bilioni 6.561 ukilinganisha na kiasi cha thamani ya dola za Marekani bilioni 5.394 kwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022|2023
Usajili huo unataraji kuzalisha ajira 226,585 ukilinganisha na ajira 53,871 kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/2023
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri ,amesema kati ya miradi hiyo asilimia 38.19 inamilikiwa na Watanzania na asilimia 42.86 ni ya wageni .
Aidha, amesema nasilimia 19. 38 ni ya ubia kati ya Watanzania na wageni .
“Kumekuwa na ongezeko la asilimia 91.60 katika usajili wa miradi ikilinganishwa na kipindi cha hadi Juni 2023 na hadi juni 2024 ambapo miradi 707 ilisajiliwa ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo miradi iliyosajiliwa ilikuwa ni 369 tu, ajira zinazotarajiwa zimeongezeka kwa asilimia 320.61 kutoka 53,871 hadi 226,585”
Aidha amesema thamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imeongezeka kwa asilimia 21.6 kutoka Dola za Marekani 5,394.83 milioni hadi Dola za Marekani milioni 6,561.09 .
Kuhusu usajili kisekta ,Teri amesema
Serikali imendelea kuboresha Kituo cha Utoaji Huduma za Mahali Pamoja kilichoko TIC kwa kuanzisha mfumo wa kusajili miradi ya uwekezaji kwa njia
ya mandao ,ambapo mfumo huo unaruhusu wawekezaji kusajili miradi yao mahali popote duniani ndani ya siku moja hadi tatu.
Mbali na hayo, Teri amesema TIC imeanzisha kampeni mbalimbali za uhamasishaji uwekezaji, ikiwemo kampeni iliyoanza August,i 2023 ikihamasisha wawekezaji wa ndani
kuja kusajili miradi yao na kituo cha Uwekezaji.
“Hili limeleta ongezeko kubwa la miradi kwa takribani asilimia 106.11 ukilinganisha na miradi ya Watanzania iliyosajiliwa katika kipindi kama hiki mwaka 2022|2023.
TIC pia kuanzia Januaril Mosi 2024 ilitanganza mwaka 2024 kama mwaka wa uwekezaji.
Pia imeweka kipaumbele katika kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na misitu”
Amesema wao kama TIC wanalenga kusajili miradi 1,000 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5 kwa mitaji ya kigeni na Dola za Marekani Bilioni 3.5 kwa mitaji ya ndani ,lakini pia wanalenga kuhakikisha kuwa asilimia 10 ya miradi inachangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa