January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIC yampongeza Rais Samia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Ruangwa

AFISA Mwandamizi Muhamasishaji wa Uwekezaji wa NdaniĀ  wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Latifa Kigoda amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kupunguza mahitaji ya kujisajili na TIC.

Kigoda ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya madini yanayofanyika katika viwanja vya soko jipya Kilimahewa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Amesema , hapo awali ilikuwa ili mwekezaji  akidhi mtaji na kujisajili na TIC lazima thamani ya mradi wake iwe milioni 200 lakini baada ya kuonekana muamko wa wazawa  kuwa ni mdogo Rais Samia akaamua kupunguza kutoka  kiasi hicho cha mtaji wa shilingi milioni 200 hadi kufikia shiingi milion 100.

Aidha ,ametumia nafasi hiyo kuwafahamisha wana Lindi na watanzania kwa ujuma kuwa kituo cha Uwekezaji wa Tanzania siyo Taasisi ya wageni kutoka nje ya nchi pekee kama wengi  wanavyodhani bali pia ni kwa ajili ya wawekezaji wazawa ambao ni watanzania wenyewe .

“Hii shilingi milioni 100 hatumaniishi kuhesabu kuanzia shiingi moja hadi milioni 100 bali tunaangalia thamani ya mradi kuanzia ardhi uliyo nayo,majengo utakayo kuwanayo kwenye mradi wako,vifaa utakavyoagiza nje ya nchi na malighafi utakazotumia, 

Kwa hiyo ukizijumilsha pamoja ndani ya miaka mitatu ukaona kwamba unafikia shilingi milioni 100 wewe unakidhi moja kwa moja kuweza kusajili mradi wako na TIC iili kuweze kupata punguzo na msamaha wa kikodi wakati unaagiza bidhaa zako za mradi kutoka nje ya nchi.”amesema Kigoda na kuongeza kuwa

“Siyo hivyo tu,lakini pia wewe kama mwekezaji una eneo akaona  uwekezaji ambao unaona haina changamoto yoyote unakaribishwa kuleta TIC ili tuweze kusaidia kutafuta mwekezwji mtakayeshirikiana kwa njia ya ubia Ili kuhakikisha kwamba mnafanikisha huo uwekezaji kwa manufaa binafsi ,wananchi na Taifa wa ujumla

Kwa upande wake Mwekezaji Mkuu wa TIC Kanda ya Mashariki Grayson Mtimba amesema kuwa wapo katika maonyesho ya madini na uwekezaji yanayofanyika katika Wilaya ya Ruangwa  Mkoani Lindi kwa ajili kufutia na   kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje wawese kuwekeza Tanzania lakini pia katika mkoa wa Lindi.

Amesema pia wao kama TIC wana jukumu  wanafanikisha uwekezaji kwakutoa vibali mbalimbali kwakushirikiana wenzao wa taasisi mbalimbali  za Serikali ikiwemo Nida  uhamiaji,osha na Taasisi nyingine ambazo zipo kituo cha mahala pamoja cha kutoa huduma zakufanikisha uwekezaji.

Aidha amesema kuwa kupitia maonyesho hao muitiko umekuwa mkubwa hasa kwa wawekezaji wa ndani ambapo wamewapa elimu ya uwekezaji na namna nawaweza kusajiri miradi TIC.

“Tunawahamasisha wawekezaji wa ndani waje wasajiri miradi yao TIC huku kuna punguzo la kodi hasa wanapoaagiza vifaa vyao kutoka nje ya nchi nasi kama TIC tupo tayari kushirikiana nao hasa wakishapata cheti cha uwekezaji kutoka TIC ikiwemo vifaa vyakuchakata madini na miradi mbalimbali”amesema Mtimba