November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIC watoa mafunzo kwa Mabalozi wa nchi mbalimbali

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Serikali kupitia kituo cha uwekezaji Nchini –TIC kimewasihi mabalozi wa Tanzania katika Nchi mbalimbali kujikita katika kutafuta fursa za uwekezaji na kuangalia maeneo ambayo kama Nchi yatanufaika nayo ikiwemo sekta ya Viwanda.

Rai hiyo ilitolewa Jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa idara ya uhamasishaji uwekezaji –TIC, John Mnali katika mafunzo na mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao wameapishwa na kupangiwa vituo hivi karibuni na Rais Dkt Samia Suluh Hassan.

“Leo tulikuwa na mafunzo mafupi na Mabalozi ambao ndiyo wawakilishi nje ya nchi na katika majukumu ambayo wanayafanya ni pamoja na Kuhamasisha Uwekezaji

Hivyo kituo Cha uwekezaji leo tumekuwa tunazungumza nao na kuwaeleza maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa na serikali katika kuweka mazingira ya kuvutia na wezeshi kwa wawekezaji wote waonakuja nchini”

Pia Mmali alisema kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimewapatia vitendea kazi Mabalozi hao ambavyo watakuwa wanavitumia katika shughuli zote za Kuhamasisha wawekezaji nchini.

Kuhusu maeneo ya uwekezaji Mnali amesema serikali imetenga maeneo ya kutosha kwa ajili wawekezaji ikiwemo kongani la viwanda lililopo wilayani Kibaha Mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine kwa kushirikiana na Halmashahuri.

“Tuna maeneo mbalimbali ambayo yana fursa za uwekezaji lakini msisitizo upo katika kuvutia wawekezaji katika maeneo ya ujenzi wa viwanda hasa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini kwasababu kupitia uwekezaji katika Sekta ya viwanda na kwa kutumia malighafi zilizotumika kwa wingi nchini, watu wengi wataweza kunufaika kupitia uwekezaji wa aina hiyo kutokana na ajira mbalimbali ambazo zitawekezwa”

Kwa upande wao baadhi ya mabalozi walioshiriki kikao hicho wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutafuta wawekezaji katika sekta mbalimbali ili kuleta tija kwa Taifa.
“Mafunzo haya yatatusaidia kwenda kutafuta wawekezaji nchini ambao watakuja kuwekeza katika Sekta mbalimbali nchini kama kilimo, madini, viwanda kwaajili ya kuongeza thamani ya mazao ambayo tunazalisha” Alisema mmoja wa Mabalozi hao

Mabalozi waliopatiwa mafunzo na –TIC ni pamoja na Balozi Joseph Sokoine Nchini Canada, Balozi Fatma Rajab Nchini Oman, Balozi Naimu Azizi Nchini Australia, Balozi Ali Mwadini Nchini Ufaransa pamoja na Na Balozi Ceasar Waitara Nchini Namibia.