January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIC ,Azania bank kuboresha ufanisi kuhudumia wawekezaji

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

KITUO Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeingia makubaliano na Benki ya Azania kwa lengo la kuboresha ufanisi wa utendaji wa kuwahudumia wawekezaji wa ndani na nje.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji wa saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi wa TIC, Gilead Teri amesema mashirikiano hayo ni mwendelezo wa maboresho hasa katika upande wa utendaji kazi wa kila siku.

“Moja ya majukumu yetu ni kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wawekezaji wa ndani na nje nyezo muhimu ni kushirikiana na wadau wengine pamoja ambao wanauwezo mkubwa kuliko sisi na wenye maarifa, na wigo mpana ambao no Benki ya Azania,”amesema Teri.
Alifafanua kuwa “Sisi kama kituo cha Uwekezaji Ili tuweze kufika mbali ni lazima tusimame katika mabenga ya watu wengine ambao ni wakubwa kuliko sisi na wenye maarifa.”

Aliupongeza Uongozi wa menejimeti ya TIC kwa utayari wa kushirikiana na Benki ya Azania kwasababu Benki hiyo inawigo mkubwa wa kuwafikia watanzania na wateja wake.

Amesema ukubwa wa Benki ya Azania na wigo wake mpana wa kuwafikia watanzania ndio jambo lililowavutia zaidi hivyo kupitia mashirikiano hayo yatasaidia kuwafikia wateja na watanzania kwa ujumla sambamba na kuwafikia wawekezaji wa nje na ndani.

“Tunatarajia mashirikiano haya yawe sehemu ya kutoa huduma katika kituo cha pamoja kwani Benki ya Azania wanayotaaluma kubwa katika masuala ya mifumo mbalimbali,”amesema Teri.

Kwa upande wake Mkurungenzi wa Sheria Benki ya Azania, Charles Mugila amesema wanayofuraha ya kufikia makubaliano hayo yaliyolenga kufikia mambo mbalimbali katika masuala ya uwekezaji.

“Tunajisikia faraja kuwa sehemu ya makubaliano haya kwani Benki hii ni ya kitanzania inamilikiwa na Taasisi za umma Kwa asilimia 99 hii ni fursa muhimu kwetu ili kufikia mambo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha uwekezaji unafika mbali zaidi,”amesema

Amesema kupitia wawekezaji wanaokuja nchini wamesaidia kuleta matokeo chanya ikiwemo kuongeza ajira sambamba na uchumi wa nchi kukua zaidi.