Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza
TAASISI yaThe Desk & Chair,imetekeleza mradi wa uchimvaji wa kusima kirefu Gereza Kuu la Butimba,mkoani Mwanza ,ili kukabiliana na changamoti ya maji katika eneo hilo.
Mradi huo,uliogharimu kiasi cha milioni 40, umelenga kutoa suluhu ya maji kwa zaidi ya watu 3,000 kila siku, wakiwemo maofisa wa gereza, askari, wafungwa, mahabusu, na familia zao.
Katika hafla ya kukabidhi mradi huo Novemba 13,2024,Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Dkt. Sibtain Meghjee, amesisitiza kuwa utapunguza kwa kiasi kikubwa adha ya ukosefu wa maji na kuboresha afya za watumiaji wa maji gerezani.
“Mradi huu utahakikisha usafi wa mazingira,kupunguza magonjwa ya ngozi na kuhara, kuboresha afya ya wafungwa,mahabusu,askari na familia zao,” amesema Dkt.Meghjee.
Kwa mujibu wa Dkt. Meghjee, kisima hicho kina urefu wa mita 100,kinatoa maji safi na salama, na mfumo wa usambazaji maji umejengwa kwa umakini kuanzia nje hadi ndani ya gereza.Ambapo mradi huo umehusisha uchimbaji wa kisima kirefu, usimikaji wa pampu ya kusukuma maji, na ufungaji wa matangi matatu yenye uwezo wa kuhifadhi lita 1,000 kila moja.
Aidha, mradi huo umejumuisha ukarabati wa tanki la lita 15,000, kuunganishwa kwa maji kwenye ofisi za gereza, na uwekaji wa mifumo ya umeme kwa ajili ya pampu,pamoja na malipo ya shilingi 550,000 za umeme wa luku.
Mbali na mradi wa maji, The Desk & Chair Foundation pia imesaidia vifaa vya elimu katika Gereza la Butimba, baada ya ombi la Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Jiji la Mwanza,ambavyo ni mbao za kufundishia, karatasi, kalamu, penseli, na majora mawili ya kushona sare za wafungwa.
Dkt. Meghjee amesema msaada huo ni juhudi za kuboresha elimu kwa wafungwa na mahabusu, ili kuwawezesha kupata ujuzi unaoweza kuwasaidia baada ya kumaliza kutumikia adhabu zao.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Masudi Kimolo, ameeleza kuwa mradi huo wa maji utaondoa kero kubwa ya ukosefu wa maji, ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa katika gereza hilo.
“Maji haya yatatumika kwa matumizi ya wafungwa, mahabusu, na familia za maofisa na askari. Pia, usafi wa mazingira na afya zao utaboreshwa. Pamoja na hayo, deni la shilingi milioni 400 linalotukabili katika gereza letu baada ya kupata mradi huu halitaongezeka,” amesema Kimolo.
Ameongeza kuwa miundombinu ya mradi huo itatunzwa kwa umakini ili kuhakikisha inakuwa endelevu kwa miaka mingi ijayo mbapo ameahidi kuchukua hatua kali kwa watakaothubutu kuharibu au kuzuia utendelevu wa mradi huo kuwa, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahalifu wa aina hiyo.
Katika hatua nyingine, Kimolo ameishukuru The Desk & Chair Foundation kwa msaada mkubwa walioutoa, akisema utaendelea kuwa na manufaa makubwa si tu kwa wafungwa, bali pia kwa askari na familia zao.
“Tunawashukuru sana kwa msaada wenu, na tunatarajia msaada zaidi katika maeneo mengine ya maendeleo.Kwa ujumla, mradi huu unaonesha juhudi za The Desk & Chair Foundationkatika kushughulikia changamoto za kijamii na kuboresha maisha ya watu, huku ukitilia mkazo katika afya, elimu, na usafi wa mazingira”,amesema.
Kimolo amesema mmsaada huo unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi binafsi, serikali, na jamii katika kutatua changamoto zinazowakumba watu wengi.
Awali Sheikh Hashimu Ramadhan, alikumbusha kuwa mradi huo wa maji unalenga kutoa msaada kwa watu waliopo gerezani, na kwamba kutoa maji ni tendo la thawabu kubwa ka mujibu wa Quran.
“Maji ni muhimu katika uhai wa kila kiumbe, na kutoa maji kwa watu ni sadaka endelevu na thawabu maradufu.”amesena Sheikh Ramadhan huku akitaja kuwa gereza ni mahali pa kujifunza, kama ilivyo katika Qur’an, na kwamba wafungwa wanastahili kupata huduma muhimu kama maji, ili waweze kuishi kwa afya bora na ustawi.
Pai mradi huo wa The Desk & Chair Foundationni mfano mzuri wa jinsi taasisi za kiraia zinavyoweza kushirikiana na serikali na jamii katika kutatua changamoto muhimu za kijamii.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote