Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Kiteto
MAKAMU Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB)Mohamed Khamis Hamad amesema kuwa haki za Binadamu zinamlenga kila mtu kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Mohamed amesema hayo Machi 27,2025 wakati akitoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa askari Polisi wa Kituo cha Kiteto.
Mohamed amesema kuwa katika Katiba ya kuanzia Ibara ya 12 hadi ya 25 imetaja haki mbalimbali ikiwemo usawa wa sheria,kutobaguliwa na nyingine ambazo kila mtu anastahili kupata
“Kwa kusema hivyo hata ninyi Polisi mna haki kama binadamu wengine,”amesema Mohamed.
Aidha,Mohamed amesisitiza kuwa Polisi wanahaki ya kutekeleza majukumu yao kadri sheria inavyowaongoza pasipo kupoteza haki ya mtuhumiwa.
“Kumekuwa na changamoto baadhi ya watu kuwabeza Askari Jeshi la Polisi na wengine kuwashambulia bila kujali kuwa na wao ni binadamu na wana haki sawa na wengine”amesema Mohamed
Pia Mohamed ametoa wito kwa wananchi kuheshimu Jeshi la Polisi kutokana kuwa wao ni walinzi wa raia na mali zao.
Kwa upande wa Askari hao wameishukuru THBUB kwa kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora ambayo italeta tija katika utendaji kazi wao.
Kwa hatua nyingine Askari hao wameomba THBUB kufikisha salam za shukran kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapandisha Madaraja Askari hao.
More Stories
Mo Dewji na Urithi anaoujenga ,unavyoenda mbali zaidi ya mafanikio binafsi
Mulika Community kusaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili
TMDA yashinda tuzo za PRST ya Umahiri katika kampeni bora ya utoaji elimu jamii