November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TGGA yamuaga kiongozi wake kuwakilisha vijana COP27

Na Penina Malundo,timesmajira

Maskauti wa kike Tanzania ( (TGGA),wamemuaga Mwanachama wake Clara Benjamin juzi kwenda  kushiriki Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika nchini Misri unaojulikana kwa jina la COP27 ikiwa na lengo la kufikisha hoja zao za kuonyesha ni namna gani mabadiliko ya tabianchi yanavyomuathiri Mwanmke na mtoto wa kike. 

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam wakati akimsindikiza Kiongozi huyo wa Tanzania Girl Guides Association ( TGGA),Wintapa Luila alisema taasisi yao imeamua kumtuma mwakilishi katika mkutano huo ikiwa na lengo la hoja zao mbalimbali ziwezs kusikika na kufanyiwa kazi.

Amesema wao kama Skaunti wanawake wamemtuma mwakilishi huyo kwa sababu  pamoja na kufanya mambo mengine pia inajishughulisha na masuala ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha inatoa elimu juu ya mabadiliko hayo yanayotokea sasa katika maeneo mengi na madhara yake kuanza kuonekana.

“Clara anaenda nchini Misri lengo likiwa kwenda kuwakilisha taasisi yetu kwani tunajishughulisha na kutoa  elimu juu ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi hivyo tunaimani hoja zetu mbalimbali nikwenda kuongelewa huku  kuwakilisha mabinti wote na wanawake watanzania kwa ujumla ambao ni wahanga namba moja wa mabadliko ya tabia nchi,”amesema 

Kwa Upande wake Meneja Mradi wa Msichana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi,Nyendo Kinyonga,amesema Clara anaenda kupaza sauti 
 ya wanawake na watoto wa kike kwani  ukiangalia masuala ya mabadiliko ya tabianchi yanamuathiri mtoto wa kike na mwanamke.”Sisi kama maskauti wa kike  Tanzania na Duniani kwa ujumla tunategemea mabinti hawa wanaoenda kutuwakilisha katika mkutano huo wa COP27  kuongelea usawa wa kijinsia katika mabadiliko ya tabianchi,”amesema na kuongeza

”Tunajua kuwa katika mfuko wa mabadiliko ya tabinchi haijaelezea kuwa wanawake wanapata asilimia ngapi na wanaaume wanapata asilimia ngapi kwahiyo wasichana hawa wanaenda na kuwa kama sehemu ya mjadala wa COP27 na hii kutokana na wao kuwa waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabinchi.,”amesema 

Amesema baada ya kumalizika kwa mkutano huu watakuja na Agenda yao  na kuona kwamba agenda zao walizoziwasilisha katika mkutano kama zimejibiwa au la na kuja na mapendelezo ambayo watayawasilisha kwa Waziiri mwenye dhamana ya Mazingira na Muungano.

Naye Mwakilishi wa Wasichana kwenye kupaza sauti katika masuala ya maamuzi yanayohusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, Clara Benjamin amesema lengo lake ni kwenda kufanya sauti ya mwanamke na msichana kusikika juu ya mabadiliko ya tabianchi kwani hilo kundi hilo ni kubwa linaloathirika na mabadiliko hayo.

”Mimi ni mwakilishi ninaenda kupaza sauti kwani kuna umuhimu wa kumuhusisha mwanamke katika matokeo yoyote ya mabadiliko ya tabianchi,…..Sisi lengo letu kubwa ni kufanya implementation ya ile mikataba mikubwa waliyopitisha ili kutupoatia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wanatakiwa kutupa sisi fund ili kupata teknolojia.

Amesema kwa sasa hivi moja ya kitu kikubwa   kinawaathiri wanawake katika madhara ya mabadiliko ya tabianchi ni suala la ukosekanaji wa maji majumbani ambapo mwanamke anaonekana kuwa mhanga mkubwa kutokana na  shughuli zote za nyumbani kuwa ni zake.