Na Esther Macha, timesmajira,Online , Rungwe
SERIKALI kupitia kampuni ya Uendelezaji wa nishati jadidifu ya Jotoardhi Tanzania (TGDC )imeanza hatua za awali za utafiti wa kuanza utekelezaji wa mradi wa kuzalisha Megawati 200 za umeme kwa kupitia nishati ya Jotoardhi katika Mikoa ya Mbeya na Songwe.
Imelezwa kuwa jotoardhi ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo chini ya uso wa dunia .
Akizungumza na waandishi wa habari wa Mikoa ya Mbeya na Songwe , mjiolojia Mwandamizi na Meneja mradi ,Albano Mahecha amesema mradi wa Jotoardhi wa Kyejo Mbaka uliopo Halmashauri ya ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ndiyo mradi wa kwanza kuanza kucholongwa visima kwa ajili ya uzalishaji wa nishati hiyo uliopo Halmashauri ya Busokelo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Mahecha amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa machi 3, mwaka huu na kwamba utekelezaji mpaka sasa kwenye shimo la kwanza wamefikia mita 70 na unatekelezwa na kampuni ya uendelezaji wa mradi wa Jotoardhi (TGDC)kwa kushirikiana na STAMICO ambayo nayo ni kampuni ya umma.
“Kiufupi lengo la mradi huu ni mwendelezo wa tafiti ambazo tunaendelea nazo tulianza na tafiti za juu na sasa tunaenda kuthibitisha tafiti za chini na kuangalia uzalishaji tunaotarajia wa mradi na kuwisha taarifa za ziada kuwepo wa uzalishaji mradi wa Kyejo _Mbaka ,mradi unaendelea vizuri na unahusisha mashimo matatu ya visima vifupi na mradi huu tunatarajia tutautekeleza na kuukamilisha ndani ya miezi mitatu”amesema Mahecha.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya uendelezaji wa Jotoiardhi (TGDC)Mhandisi ,Kato Kabaka amesema kuwa miradi hiyo nishati jotoardhi inatekelezwa eneo la Ziwa Ngosi,Mto Songwe na Kyejo Mbaka uliopo wilayani Rungwe katika Halmashauri ya Busokelo.
Aidha Mhandisi Kabaka amesema kuwa ucholongaji ni sehemu ya utafiti kujua kwamba walichofikiria katika utafiti wa awali ndivyo kilivyo na bahati nzuri walivyochoronga wamekuta maji ya moto kwenye kina kifupi na uchorongaji unaendelea.
Amesema kuwa shughuli inayoendelea ni kuthibiti maji ya moto ili kazi iweze kuendelea na wataalam wa kuthibiti maji ya moto tayari wapo na vifaa na kazi.
Naye Mkurugenzi wa maendeleo wa Biashara (TGDC) Mhandisi Shakiru Kajugus amesema kuwa mradi huo wa visima vitatu umefikia awamu ya kutekeleza zoezi linaloendelea katika mradi huo ni utafiti wa awali wa mradi unaoendelea wa kupata kiwango sahihi cha uwingi wa jotoardi katika maji na uchorongaji wa visima .
Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mbeya na Songwe ni miongoni mwa wadau wa kwanza ambao wamepata fursa ya kutembelea miradi hiyo, kwalengo la kuhabarisha umma juu ya uwepo wa miradi hiyo nchini.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia