December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

TFF yazitaka klabu za mpira wa miguu kufanya usajili kabla dirisha kufungwa

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF, limezitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Daraja la pili, na Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite, kufanya usajili kwa wakati kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Klabu za Ligi Kuu zinatakiwa kufanya usajili wa wachezaji wa timu ya wakubwa, chini ya umri wa miaka 20 na wale wa chini ya miaka 17.

Kwa upande wa Ligi daraja la kwanza na la Pili, wanatakiwa kufanya usajili wa timu za wakubwa pamoja na chini ya miaka 17, wakati kwa wanawake watasajili timu moja ambayo inaweza kuwa na mchanganyiko wa umri.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Agosti 31 saa 5:59 usiku na hakutakuwa na muda wa ziada. Hivyo TFF inaendelea kukumbusha
Klabu yoyote yenye changamoto kuwasiliana n Idara ya Mawasiliano TFF.