December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu 28.09.2020

N’Golo Kante

Manchester United imewasiliana na washauri wa kiungo mkabaji wa Chelsea N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 29 raia wa Ufaransa kuhusu hatua ya kuondoka klabu hiyo, lakini makubaliano yoyote na mchezaji huyo, huenda yakapelekea kupunguzwa pakubwa kwa mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki. (Mirror).

Lazio huenda ikataka kuwasajili viungo wawili wa Manchester United, Juan Mata, 32, na Mbrazili Andreas Pereira, 24. (Sun)

Leicester City wanapanga kumsajili beki wa kati wa Torino, 23, Mbrazili Gleison Bremer, ambaye pia anawindwa na klabu ya Everton. (Football Insider)

Joshua King

Mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Joshua King, mwenye umri wa miaka 28 anawindwa na Tottenham Hotspur wakati huu ambapo klabu hiyo inataka kumsajili mshambuliaji kabla ya siku ya ukomo wa uhamisho. (Telegraph )

Spurs pia wanapiga hesabu za kumsajili Kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya Taifa ya Uswizi Haris Seferovic, mwenye umri wa miaka 28. (Football Insider)

%%%%%%%%%%%%%%%