July 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matteo Guendouzi

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu 05.10.2020

Matteo Guendouzi

Kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, mwenye umri wa miaka 21, anatarajiwa kuelekea katika timu ya ligi ya Bundesliga Hertha Berlin, baada ya kuachwa nje ya kikosi cha timu hiyo katika uwanja wa Emirates. (Mirror)

Tottenham inatarajiwa kufanya jaribio la mwisho kumsaini beki wa InterMilan mwenye umri wa miaka 25 raia wa Slovakia Milan Skriniar. (Mirror)

Klabu ya Juventus inaandaa dau la kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emmerson Palmieri wakiwa na lengo la kumsaini mchezaji huyo wa Itali mwenye umri wa miaka 26 kwa. (Calciomercato – in Italian)

Thomas partey

Arsenal imefutulia mbali mpango wao wa kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Atletico Madrid Thomas Partey, mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ghana. The Gunners haiko tayari kuafikia kifungu cha kumnunua mchezaji huyo cha pauni milioni 45. (Mirror)

Sheffield United inajiandaa kuipiku West Brom kumsajili mchezaji wa klabu ya Metz na Senegal mwenye umri wa miaka 25 Habib. (Le 10 Sport – in French)

Beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, mwenye umri wa miaka 20, huenda anaondoka Barcelona kwa mkopo, akitarajiwa kuelekea Fulham a huku Everton pia nayo ikiwa ina hamu ya. kumsajili beki huyo. (Le 10 Sport – in French)

Douglas Costa

Bayern Munich inamnyemelea winga wa Juventus raia wa Brazil Douglas Costa mwenye umri wa miaka, 30, iwapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19. (Kicker – in German)

Celtic ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham Robert Snodgrass, mwenye umri wa miaka33 kwa mkopo lakini pia wako tayari kwa makubaliano ya kudumu.. (Sun)

Uhamisho wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger kuelekea AC Milan unaelekea kutimia , huku Chelsea ikifurahia kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kabla ya mjadiliano ya kumuongozea kandarasi , huku akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake. (90min)

Anderlecht inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na raia wa Ireland Josh Cullen, 24. (Het Laatste Nieuws – in Dutch)

Brighton inaandaa dau la Euro milioni 11.5 sawa na (£10.4m) kumnunua kiungo wa kati wa Poland Jakub Moder, mwenye umri wa miaka 21, kabla ya kumuuza kwa mkopo kwa Lech Poznan kwa msimu huu. (Super Express – in Polish)

Geoffrey Kondogbia

Kiungo wa kati klabu ya Valencia na jamhuri ya Afrika ya kati Geoffrey Kondogbia, 27, ananyatiwa na klabu isiojulikana kwa dau la pauni milioni 22m.(Marca – in Spanish)

Winga wa Roma raia wa Uholanzi Justin Kluivert, mwenye umri wa miaka 21, anaelekea RB Leipzig kwa mkopo wa muda mrefu (Fabrizio Romano via Football Italia)

Klabu ya Paris St-Germain imewasilisha ombi la kumnunua kwa mkopo beki wa Porto na Portugal Danilo Pereira, 29. (Goal)

Kiungo mshambuliaji wa Werder Bremen Davy Klaassen, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kurudi katika klabu yake ya utotoni Ajax, baada ya dau la pauni milioni 10 kuafikiwa ili kumsajili mchezaji huyo wa Uholanzi. (De Telegraaf – in Dutch)

Mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, mwenye umri wa miaka 31, atasaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Bayern Munich, baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Kicker via Goal)