Antonio Rudiger
KLABU ya Barcelona na AC Milan wanapigana vikumbo kuwania saini ya beki wa kati wa Chelsea, Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujeruman.(ESPN, via Sport, Calciomercato – in Italian)
Klabu ya ligi kuu Marekani inaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumnasa kiungo wa kati Mjerumani anayekipiga Arsenal Mesut Ozil, mwenye umri wa miaka 32. (DHA-in Turkish)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga ameiambia klabu ya Rennes kuwa anataka kuondoka msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anavutiwa na Manchester United.(Mundo Deportivo via Sun)
Juventus wanaweza kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey msimu ujao baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, kushindwa kuisaidia klabu yake tangu ajiunge nayo akitokea Arsenal mwaka 2019. (Mail)
Mshambuliaji wa Brazil Hulk, mwenye umri wa miaka 34, anaweza kujiunga na klabu ya Ligi Kuu England kwa uhamisho huru mwezi Januari baada ya kumaliza mkataba wa miaka minne na Shanghai SIPG ya China. (Sun)
Kurejea kwa Samuel Umtiti katika kikosi cha Barcelona baada ya kujeruhiwa ni hatua moja nyingine kuelekea kuiacha klabu hiyo mwezi January, wakati Everton na Juventus zote zikivutiwa na mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi, mwenye umri wa miaka 27. (Sport – in Spanish)
Mshambuliaji wa Everton ya Italia Moise Kean, mwenye umri wa miaka 20, amefungua milango kwa uhamisho wa kudumu kuelekea Paris St-Germain baada ya kuanza vyema na mabingwa hao wa ufaransa. (Goal)
Leeds United wameendelea kumfuatilia Marcus Edwards,22, baada ya winga huyo wa kushoto kuondoka Tottenham na kujiunga na Vitoria Guimaraes ya Ureno mwaka 2019.(Football Insider)
Klabu kadhaa Ligi Kuu England zinavutiwa na kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Vesga, mwenye umri wa miaka 27, ambaye mkataba wake na Athletic Bilbao utakamilika msimu ujao.(AS – in Spanish)
Bristol City ni miongoni mwa vilabukadhaa vinavyopanga uhamisho kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto George Cox, mwenye umri wa miaka 22, aliyekuwa kwa uhamisho wa kudumu akitokea Brighton kwenda Fortuna Sittard ya Uholanzi msimu uliopita.(Football Insider)
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes