January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Christian Ericsen

Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne 10.11.2020

Christian Ericsen

Klabu ya Tottenham Spurs, wamepewa nafasi ya kumsajili tena kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Inter Milan. (Football Insider)

Hata hivyo klabu hiyo, huenda wakapewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 31, kwa mkataba wa kudumu kutoka Real Madrid kwa ka kitita cha euro milioni 15 (£13.4m) (Mundo Deportivo – in Spanish)

Manchester United wamesitisha uamuzi kuhusu hatma ya kipa Sergio Romero, mwenye umri wa miaka 33 raia wa Argentina hadi pale mpango wa kumuuza Dean Henderson utakapokamilika, huku Muingereza huyo akiwa katika oradha ya uhamisho wa mkopo mwezi Januari. (ESPN)

Olivier Giroud anatafakari kuhusu maisha ya baadae katika klabu ya Chelsea. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, aliyewahi kuhusishwa na klabu ya Inter Milan, huenda akahamia mahali ambapo patamhakikishia kujiunga na kikosi cha Ufaransa msimu ujao. (Football London)

Manchester United huenda wakamkosa Ousmane Dembele mwezi Januari, huku Barcelona ikijiandaa kumpatia mshambuliaji huyo wa Ufaransa jukumu kubwa baada ya Ansu Fati kuumia (Sport – in Spanish)

Jaribio la Chelsea la kumsajili mlinzi wa zamani wa Nottingham Forest Anel Ahmedhodzic kutoka Malmo zinazibwa kwa mujibu wa baba yake kiungo huyo raia wa Bosnia .

Manchester United imemzuia mlinzi wao Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 26, kujiunga na kikosi cha Sweden kwa mechi ya kirafiki na Denmark kutokana na masharti ya usafiri ya Covid-19 yanayotekelezwa kwa sasa na Uingereza. (Goal)

Manchester United inatafakari kuwapa uhamisho wa mkopo wachezaji wake watatu – kiungo wa kati wa Ireland Kaskazini Ethan Galbraith, kiungo wa kati wa Mhispania Arnau Puigmal na beki Ethan Laird -dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari. (Manchester Evening News)

Liverpool imefunga kambi yao ya mazoezi ambayo wamekuwa wakitumia kwa zaidi ya miaka 60, Melwood. (Liverpool Echo)

%%%%%%%%%%%%