Ousmane Dembele
Manchester United wako kwenye mazungumzo makali ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Ufaransa (Daily Record).
Huku Man United wakipuuza kuhusishwa kuhusishwa na mchezaji huyo.
Dele Alli
KLABU ya Paris St-Germain (PSG), wana uhakika kuwa kiungo wa Tottenham Hotspur Dele Alli, mwenye umri wa miaka 24 raia wa England, anataka kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail)
Max Aarons
Mlinzi wa Norwich City Muingereza Max Aarons, mwenye umri wa miaka 20, amekubali mkataba wa miaka mitano kujiunga na Barcelona. (Sport – in Spanish).
Mateo Guendouzi
Kiungo wa Klabu ya Arsenal mwenye umri wa miaka 21 raia wa Ufaransa Matteo Guendouzi, ameomba kuondoka klabuni hapo. (Tribal Football)
KLABU ya Borussia Dortmund wana uhakika winga wao Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20 raia wa England, hataondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa usajili, licha ya kuhusishwa na Manchester United. (Independent).
Nayo klabu ya Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Napoli raia wa Poland mwenye umri wa miaka 26, Arkadiusz Milik, kuhitumikia klabu hiyo. (Corriere dello Sport – in Italian)
Klabu ya Southampton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati raia wa England Tom Davies kutoka Everton. (Talksport)
Arsenal imepata mpinzani wa klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa Ulaya, katika mbio zake za kumwania kiungo wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph – subscription required)
Kipa wa Manchester United Sergio Romero, mwenye umri wa miaka 33, raia wa Argentina anataka kuondoka kwenye klabu hiyo. (Sun)
Antonio Rudiger
Mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 27, raia wa Ujerumani, anaangalia hatma yake katika klabu hiyo, baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza. (Sky Sports)
Mlinzi wa Bayer Leverkusen, mjerumani Jonathan Tah, mwenye umri wa miaka 24, hayuko kwenye orodha muhimu ya wachezaji wanaowaniwa na Leicester City.(Kicker – in German)
Klabu ya Fulham wanajaribu kumsajili kwa mkopo winga wa zamani wa Everton na Charlton Ademola Lookman. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anachezea RB Leipzig. (Evening Standard)
Jesse Lingard
Kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 27, hatajiunga na Tottenham licha ya kuhusishwa kwake kutaka kuhamia timu hiyo. (Athletic – via Twitter)
Hata hivyo Man United wapo mbioni kumuongezea mkataba hadi mwaka mmoja Lingard ili kutunza thamani yake ya pauni milioni 25. (Sun)
Winga wa Southampton, raia wa Morocco Sofiane Boufal, mwenye umri wa miaka 27, anawaniwa na klabu ya Ufaransa ya Angers. (L’Equipe, via Daily Echo)
Naye Winga wa Wales Daniel James, mwenye umri wa miaka 22, huenda asiondoke Manchester United msimu huu, licha ya kuhusishwa na Leeds United. (Manchester Evening News)
%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM